Ujumbe wa kidini kutoka katika mji wa Karkal India wakutana na ugeni kutoka katika Ataba tukufu utakao shiriki kwenye kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s) na wasisitiza kua awamu hii itakua ya pekee…

Maoni katika picha
Ujumbe wa kidini kutoka katika mji wa Karkal uliopo kaskazini ya India umewatembelea wageni kutoka katika Ataba tukufu walio wasili asubuhi ya leo Juma Nne (03 Aprili 2018m) sawa na (16 Rajabu 1439h), wanao tarajiwa kushiriki kwenye kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) awamu ya sita, litakalo husisha ugeni kutoka katika Atabatu Husseiniyya, Askariyya na wasimamizi wa kongamano, Atabatu Abbasiyya tukufu, kongamano litakua na kauli mbiu isemayo (Amirul Mu-uminina (a.s) ni wa mwanzo wa wenye kuabudu na mwenye zuhudi zaidi katika wenye zuhudi) litakalo fanyika katika hauza ya Ithna Ashariyya katika mji tajwa hapo juu, siku ya Alkhamisi ijayo Inshallah na litakua la siku tatu, litakua na vitu mbalimbali kama ilivyo pangwa na kamati ya maandalizi.

Ujumbe ulio watembelea unaongozwa na Shekh Abdullahi Najafi akiwa na jopo la wanachuoni kutoka katika mji huo ambao upo umbali mkubwa kutoka sehemu walipo wageni wa Ataba tukufu katika mji wa Lahalah Daru, panakadiriwa kuna kiasi cha zaidi ya milo meta (200), aliueleza ugeni wa Ataba tukufu kuhusu furaha yake kwa mkutano huu na kwa kuchagua kongamano lifanyike katika mji huu, wakasisitiza kua awamu hii kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) itakua zuri na litaendana na jina la Amirul Mu-uminina (a.s) na mwenendo wake, wakazi wa mji huu wanalikaribisha kwa furaha kubwa tukio hili la kihistoria ambalo litaingia katika kurasa za historia ya mji huu unao julikana kwa kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume na Maimamu wa Ahlulbait (a.s), hali kadhalika ujumbe huo, ulisema kua umekamilisha maandalizi yote ya kongamano hili na wamesha ondoa vikwazo vyote.

Pia ujumbe huo ulipewa maelezo kuhusu harakati za Ataba tukufu za Iraq na maendeleo yanayo shuhudiwa katika Ataba hizo ya kiujenzi, kitamaduni na kielimu ndani na nje ya Iraq, ikiwa ni pamoja na mikutano ya aina hii ianyo fanyika kati yao na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) sehemu mbalimbali za dunia ikiwa ni pamoja na India, ambayo wasimamizi wake wamehakikisha kongamano hili linakua endelezu.

Kwa upande mwingine kamati ya maandalizi ya kongamano inaendelea na shughuli zake, na tayali wamesha kamilisha maandalizi kwa kiasi kikubwa, kongamano litakua na vipengele vingi vinavyo husu utukufu wa Amirul Mu-uminina (a.s), na vinavyo linda mafanikio yaliyo patikana katika kongamano lililo pita la tano, mji wa (Karkal) ni sehemu ya kituo cha safari ndefu kuelekea miji mingine ya India kwa ajili ya kupanua wigo wa mawasiliano na wapenzi wa Ahlulbait katika miji yote ya India, ili wapenzi wa Ahlulbait (a.s) waweze kuzifahamu Ataba tukufu za Iraq kupitia kongamano hili.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s), hufanywa kwa ajili ya kuwaadhimisha Ahlulbait (a.s), na kusambaza tamaduni zao na mwenendo wao wa haki pamoja na historia yao tukufu iliyo fundisha dunia maana ya uislamu wa kweli, na kuonyesha nafasi ya Ataba tukufu za Iraq, katika kufanya na kusimamia makongamano, nadwa na mikutano mbalimbali ya ndani na nje ya Iraq, kupitia shughuli hizo zinakua zimefungua milango ya kuwasiliana moja kwa moja na watu wa tabaka tofauti katika jamii na kuielezea madhehebu ya haki, na kufafanua hatua za ujenzi na muundo wa uongozi wa kisheria wa Ataba tukufu, na vipi wameweza kua vinara na mfano mwema katika sekta zote ndani ya muda mfupi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: