Atabatu Abbasiyya tukufu yaweka mapambo meusi na yatengeneza upya sistim ya umeme katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake…

Maoni katika picha
Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Sayyid Ahmadi Swafi, mafundi wa kitemgo cha uangalizi wa haram katika Ataba tukufu na wenzao watumishi wa vitengo vingine, wamemaliza hatua ya nne ya matengenezo katika malalo ya bibi Zainabu bint Ali bun Abu Twalib (a.s).

Hatua hii imemalizika sambamba na kumbukumbu ya kifo chake (a.s), jambo ambalo limesababisha watumushi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), waweke mapambo yanayo ashiria huzuni katika malalo yake tukufu, na kueneza mapambo meusi katika kaburi, uwanja wa haram na kubba tukufu.

Kiongozi wa ugeni ulio kwenda katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) bwana Hassan Hilali ambaye ni rais wa kitengo cha uangalizi wa haram ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mafundi wetu wamefanikiwa kuendelea na hatua ya nne ya ukarabati wa haram tukufu ya bibi Zainabu (a.s), wameweka waya wa umeme wenye urefu wa mita (10000) ulio tengenezwa Italia, na wenye unene wa (milimita 600) na wamefunga mbao zilizo tengenezwa Ufaransa zenye ukubwa wa (sm180*120), wamefanya kazi usiku na mchana, wamemaliza kazi ya kuunganisha umeme wa malalo tukufu kutoka katika kituo cha pili hadi kituo kikuu, ndani ya muda ulio pangwa, ndani ya siku tano tu tumefanya kazi ya miezi minne katika miradi mingine”.

Akaongeza kusema kua: “Hali kadhalika wamefunga taa zenye mwanga mweupe na zenye mwanga mwekundu ndani ya uwanja wa haram tukufu wa bibi Zainabu (a.s), taa nyekundu zitakua zinawashwa katika siku za huzuni, ambazo ni siku za kumbukumbu za vifo hususan sasa hivi tunaishi katika kipindi cha kumbukumbu ya kifo cha bibi Zainabu (a.s), na taa nyeupe zinakua zinawashwa katika siku za kawaida, hivi sasa kaburi tukufu limepambwa na vitambaa vyeusi pamoja na kwenye kubba tukufu na ndani ya uwanja wa haram, baada ya mafundi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu kuchukua vipimo kamili kwa kaburi, kubba na maeneo ya jirani na sehemu hizo”.

Kazi iliyo fanywa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ni yakujivunia, inasifiwa na watu wa karibu na wa mbali, baada ya kufanya kazi usiku na mchana, kwa kufuata maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuandaa chumba maalumu cha kukontroo sistim ya umeme, baada ya kutokuwepo chumba kama hicho hapo awali, pia wameandaa mabango yenye ujumbe unao husu Maimamu watukufu, yatakayo kua yanawekwa katika siku za kumbukumbu za uzawa au vifo vya Maimamu watakasifu na matukio ya kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: