Watu wa kitongoji cha Bashkum waukaribisha ugeni wa Ataba tukufu za Iraq na hisia zao hazielezeki…

Maoni katika picha
Kitongoji cha Bashkum kilichopo katika mji wa Karkal India ni moja ya sehemu walizo simama wageni kutoka katika Ataba tukufu za Iraq watakao shiriki katika kongamano la Amirul Mu-minina (a.s) litakalo anza Alkhamisi ya kesho chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirul Mu-uminina (a.s) ni wa mwanzo katika wenye kuabudu na mwenye zuhudi zaidi katika wenye zuhudi), litakalo fanyika kwenye hauza ya Ithna ashariyya katika mji tajwa hapo juu, na litadumu suku tatu, kongamano hilo litahudhuriwa na wawakilishi wa Atabatu Husseiniyya, Askariyya na Atabatu Abbasiyya ambao ndio wasimamizi wa kongamano hilo.

Miongoni mwa wenyeji walio pokea ugeni huo ni Shekh Hussein Muqaddas ambaye ni mwanachuoni mkubwa wa mji huo, mapokezi yalikua makubwa sana, wakazi walijitokeza kwa wingi na wakakusanyika katika Msikiti na Husseiniyya, wakionyesha hisia za mapenzi ya hali ya juu kabisa kwa wageni ambayo hayaelezeki, kutokana na heshima yao pamoja na mapenzi makubwa waliyo nayo kwa maeneo matukufu ambayo umetoka ugeni huu.

Katika sherehe za mapokezi hayo, ugeni ulitoa tamko la shukrani lililo wasilishwa na Shekh Baasim Abdali kutoka katika kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alianza kwa kutoa shukrani kutokana na mapokezi mazuri na hisia za mapenzi ya hali ya juu kwa maimamu wa Ahlulbait (a.s), akabainisha kua: Sisi tumekuja kutoka katika ardhi ya Shahada Karbala ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutoka katika ardhi ya Askariyyain (a.s), kukufikishieni japo kidogo miongoni mwa baraka za miji hiyo, kwa utukufu na baraka za maimamu (a.s) tumekufikieni, na kukutana na nyuso hizi tukufu zenye nuru itokanayo na mapenzi ya Ahlulbait (a.s), hongereni sana kwa mapenzi haya kwa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s), tena mmeyatafsiri katika uhalisia kwa kujenga maelewano baina yenu pamoja na watu wa tabaka zote, akamaliza kwa kusoma dua’u Faraj.

Wakazi wa kitongoji hicho walielezea furaha kubwa waliyo kua nayo kwa kuwaona watumishi wa Ataba tukufu za Iraq, kwa kipindi kifupi chenye thamani kubwa na maana kubwa sana kwao.

Kamera ya mtandao wa kimataifa Alkafeel ilikuwepo katika sherehe za mapokezi hayo, ilifanikiwa kupiga picha chache zinazo onyesha nyuso za furaha ya hali ya juu waliyo kua nayo watu hao kwa kukutana na watumishi wa malalo tukufu za Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: