Baada ya kipita miezi mitatu tangu watambue kufanyika kwa kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita katika mji wao, watu wa mji wa Karkal India na vitongoji vinavyo uzunguka walikaa usiku na mchana wakisubiri kufika siku hiyo na kushuhudia halfa ya kongamano hilo, kadri muda unavyo karibia na walipo sikia ujio wa wageni kutoka katika Atabatu Husseiniyya, Askariyya pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ndio wasimamizi wa kongamano hili, wametoka kwa wingi sana, watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume, vijana kwa wazee, wameacha kazi zao za kila siku na kwenda kuwapokea wageni hao, wametembea makumi wa kilometa wakipita katika njia zenye mazingira magumu, kuanzia mji wa Lahalah Daru hadi katika mji wa Karkal ambao upo umbali wa kilometa (200), pamoja na wapokezi waliopanda vyombo vya usafiri, kwa hakika mapokezi ni makubwa sana, hii inatokana na mapenzi yao kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ambayo yametafsiriwa na machozi ya furaha na vifijo, haya ni mapokezi makubwa sana kushuhudiwa katika miji hii kwa miaka mingi.
Wageni hao walipo fika katika mji huo na kukanyaga ardhi ya Hauza ya Ithna ashariyya mwenyezi wa kongamano hilo, litakalo anza asubuhi ya kesho Alkhamisi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, zilisikika sauti za nderemo na vifijo zikishangilia kuwasiri kwao, Shekh Baasim Abdali kutoka katika kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu akatoa shukrani kwaniaba ya wageni kutokana na mapokezi makubwa waliyo pewa, yanayo onyesha namna walivyo shikamana na dini yao pamoja na Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), akawahimiza kuendelea na mwenendo huo mtukufu, akawaambia kua tumekuja kutoka katika Ataba tukufu za Iraq, kushirikiana na nyie kiroho na kifikra na tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe kwa hilo.
Pia wakazi wa mji huo walitoa neno la ukaribisho lililo wasilishwa na Shekh Nadhir Mahdi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika watu wa mji wa Karkal katika mkoa wa Jambun na Kashmir India pamoja na wanachuoni wao na hauza zao, wanamapokezi bora zaidi, hutandika maua katika ardhi wanapo kuja wageni kutoka katika Ataba tukufu za Iraq, tunakuambieni mpo katika taifa lenu la pili mbele ya ndugu zenu wapenzi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu mtukufu na watumishi wa Ataba za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwa ujio wenu.