Kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkauthar katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimefanya nadwa ya kiutamaduni kwa wanafunzi wa chuo hicho na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya walimu wao, nadwa hiyo imefanyiwa ndani ya ukumbi mkubwa wa chuo hicho, na ilikua na mihadhara miwili, muhadhara wa kwanza ulitolewa na mtaalamu wa historia Saidi Rashidi Zamizam kiongozi wa idara ya makumbusho ya Imamu Hussein (a.s), alizungumzia historia ya mji wa Karbala na hatua za ujenzi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na hatua za uadui dhidi yake (Ataba mbili).
Kisha ukafuata muhadhara wa mtafiti Jassaam Muhammad Saidi mkuu wa kituo cha Alkafeel cha utamaduni na matangazo ya kimataifa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alizungumzia baadhi ya uzowefu wa kijamii, unao changia katika kumjenga mtu kwa ujumla, pamoja na mchango wa waumini hata kama wakiwa katika mazingira magumu kiasi gani.
Akabainisha kua: “Athari ya kuwategemea Ahlulbait (a.s) katika kutawassal kwa Mwenyezi Mungu na kuomba utatuzi wa matatizo yanayo mkumba mwanadamu, na kuamini uombezi wao ni njia kubwa ya kumaliza matatizo”.
Nadwa hii imefanyika baada ya kumaliza ratiba ya wiki ya msimu wa Karbala (Nasimu Karbala) ambayo husimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu na kushiriki Atabatu Abbasiyya kwa mwaka wa tano mfululizo.