Rais wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu awaambia wageni wa kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s): Ali (a.s) ni hema linalo tukusanya wote, pamoja na umbali na kutofautiana kwa lugha, mitazamo na madhehebu…

Maoni katika picha
Rais wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdulhussein amesema kua Imamu Ali (a.s) ni hema linalo tukusanya wote, pamoja na umbali uliopo na kutofautiana kwa lugha, mitazamo na madhehebu, kinacho tukusanya na kutufanya kua kitu kimoja ni mapenzi na ubinadamu pamoja na akili.

Ameyasema haya katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, linalo simamiwa na kuendeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Karkal kaskazini ya India na kushiriki Ataba tukufu za Iraq (Husseiniyya na Askariyya), asubuhi ya Alkhamisi (18 Rajabu 1439h) sawa na (05 Aprili 2018m), linalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Amirul Mu-minina (a.s) ni wa mwanzo katika wenye kuabudu na mwenye zuhudi zaidi katika wenye zuhudi) kwenye hauza ya Ithna ashariyya katika mji tajwa hapo juu.

Akaongeza kusema kua: “Kwanza kabisa nakufikishieni salamu kutoka kwa viongozi wakuu wawili wa kisheria wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na salamu za makatibu wakuu wa Ataba tukufu za Iraq na watumishi wote wanao fanya kazi katika malalo matukufu ya Ahlubait (a.s), hakika ni utukufu mkubwa kwetu kukutana na ndugu zetu wapenzi raia wa India, nchi hii inahistoria ndefu”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika umefika wakati wa mkutano wetu wa kila mwaka, leo tunakutana kwa mwaka wa sita mfululizo, Imamu Ali (a.s) anatukusanya katika kumbukumbu ya mazazi yake matukufu, Mwenyezi Mungu ametuwezesha kufanya kongamano hili tukufu chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya na mchango mkubwa wa Ataba tukufu za Iraq”.

Yasiri akabainisha kua: “Kongamano hili linamuangazia mtu ambaye akili na kalamu zimeshindwa kujua siri yake, kwa nini isiwe hivyo wakati Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema kuhusu yeye kua: (Ewe Ali hakuna anaye mjua Allah ispokua mimi na wewe, na hakuna anaye nijua ispokua Allah na wewe, na hakuna anaye kujua ispokua Allah na mimi) hivyo sisi ni wapungufu hatuwezi kumjua ukweli wa kumjua (a.s), lakini japo kidogo tunajaribu kuogelea katika bahari yake ya kina ili tupate japo radhi yake”.

Akaendelea kusema kua: “Mnajua kua kongamano hili linafanyika hapa India kwa mara ya sita mfululizo, mara ya kwanza lilifanyika mwaka (2013m) na (2014m) katika mji wa Lakau, na mwaka (2015m) likafanyika katika mji wa Haidar-abad, na mwaka (2016m) katika mji wa Bangolur, na mwaka wa (2017m) katika mji wa Kalkata, na mwaka huu umeteuliwa mji wenu wa Karkal, ambapo tunafanya hafla hii inayo lingania mapenzi na kuishi kwa undugu na maelewano na watu wengine, pamoja na kukubali mawazo na maoni ya wengine na kujitenga na chuki na ubaguzi”.

Yasiri pia alitoa shukrani kwa niaba ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa wakazi wote wa mji wa Karkal kwa mapokezi mazuri, na kujitolea kwao mambo mbalimbali yaliyo wezesha kongamano hili, na namna walivyo fatilia kibali cha kuruhusiwa rasmi kongamano hili, akasema: sitawasahau walio simama pamoja na sisi kwa kufanya mawasiliano mfululizo kwa ajili ya kufanikisha kongamano hili, pia shukrani za pekee kwa Ataba tukufu kwa msaada na ushiriki wao mkubwa na kamati ya maandalizi ya kongamano pamoja na watumishi wote wa Ataba tukufu, kwa kudumisha mawasiliano na kuendeleza kungamano hili, kutokea hapa katika mji huu tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ailinde jamhuri ya India pamoja na nchi zote zenye mapenzi na uislamu na awadumishie neema ya amani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: