Rais wa Jumuiya ya wanachuoni wa Ithna ashariyya: Uwepo wa ugeni unao wakilisha Ataba tukufu za Iraq ni jambo la kihistoria litakalo andikwa kwa herufi za nuru katika historia ya mji wa Karkal…

Maoni katika picha
Katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita lililo anza asubuhi ya leo (17 Rajabu 1439h) sawa na (05 Aprili 2018m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirul Mu-uminina (a.s) ni wa mwanzo katika wenye kuabudu na mwenye zuhudi zaidi katika wenye zuhudi) kwenye hauza ya Ithna Ashariyya katika mji wa Karkal, kulikua na ujumbe wa rais wa jumuiya ya wanachuoni wa Ithna Ashariyya Shekh Nadhir Mahdi Muhammadi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Leo tuna wageni watukufu sana kwetu wametoka katika nchi tukufu ya Iraq, wamewakilisha Ataba takatifu, siku hii ina umaalumu rasmi tofauti na siku zingine, hakika tunajivunia kwa kuwahudumia watumishi wa Ataba tukufu za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), hakika mji wetu umenawirika kwa kupata wageni hawa, hii yote inatokana na baraka za Maimamu (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kuwahudumia na tufanikishe kongamano hili tukufu linalo itwa jina la Amirul Mu-uminina Ali (a.s), kongamano hili tunalizingatia kua ni ujumbe kutoka kwake, yeye ndiye aliye kutumeni mje kwetu, tukio hili la kihistoria halita futika vichwani kwetu, litaandikwa kwa nuru katika historia ya mji huu, tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwasiliana nasi kwa ajili ya kufanyika kwa kongamano hili hapa India”.

Akaongeza kusema kua: “Tunawakaribisha sana wageni kutoka katika Ataba tukufu za Iraq katika mji huu, wengi wetu wamesha tembelea Ataba za Iraq, lakini pia kuna wakazi wengi wa mji huu hawajabahatika kutembelea Ataba za Karbala na maeneo mengine, leo hii watumishi wa Ataba hizo wamekuja katika mji wetu wa Karkal kuwatembelea wapenzi wa Ahlulbait (a.s), na kuwafanya watabaruku na Ataba hizo na kuwafanya waishi katika mazingira ya kiroho kana kwamba wapo katika malalo za Ahlulbait (a.s)”.

Akasema: “Sisi wakazi wa mji huu tupo tayali kubeba majukumu yote ya kuwahudumia wageni wetu watukufu katika siku hizi za kongamano tukufu, ninawashukuru sana watumishi wa Ataba tukufu kwa kuuchagua mji wetu kua mwenyeji wa kongamano hili, huu ni utukufu mkubwa kwetu na kwa mji wetu, na ninatoa shukrani kwa wakazi wa mji wa Karkal kwa ushirikiano wao mkubwa na kujitokeza kwa wingi mno katika kongamano hili, walipo sikia kua kuna wageni kutoka katika Ataba tukufu, wamejitokeza kwa wingi kuja kuwapokea na wamehudhuria kwa wingi katika kongamano hili, muendelee kuja kwa wingi ili mpate baraka za wageni hawa watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: