Ahlusunna waljamaa wa Karkal: Tunajivunia uwepo wa ujumbe wa Ataba tukufu pamoja nasi, na Imamu Ali (a.s) ni mfano bora kwa watu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Shekh Taslim Aarif amesema kua Imamu Ali (a.s) ni mfano bora kwa watu katika imani, jihadi, ukweli na msimamo, baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), na tunajivunia wageni wanao wakilisha Ataba tukufu za Iraq.

Aliyasema hayo katika ujumbe alio wasilisha kwa niaba ya Ahlusunna waljamaa waishio katika mji wa Karkal kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, lililo anza leo asubuhi (18 Rajabu 1439h) sawa na (05 Aprili 2018m) katika hauza ya Ithna Ashariyya katika mji tajwa hapo juu.

Akaongeza kusema kua: “Kama alivyo Imamu Ali (a.s) kua ni wa watu wote, na kila anaye mfuata hua hivyo, uwepo wa wageni wanao wakilisha Ataba tukufu unathibitisha maneno haya, hakika aliwapa waislamu mwongozo bora kabisa kupitia mwenendo na elimu yake ambayo aliitafsiri katika mazingira halisi”.

Kisha Shekh Aarif akasoma baadhi za hadithi zinazo onyesha utukufu wa Imamu Ali na watu wa nyumbani kwake (a.s), akasema kua: “(Siku moja) Mtume (s.a.w.w) alikua amelala katika nyumba ya Ali (a.s), Imamu Hassan (a.s) akaamka kutoka usingizini na akaomba maziwa, Akainuka Fatuma (a.s), walikua na mbuzi asiye kua na maziwa, bibi Zaharaa akaenda kumkamua mbuzi huyo na akatoa maziwa, Hussein naye akaamka na akaomba maziwa pia, Mtume (s.a.w.w) akasema aliye anza kuomba ndio aanze kunywa, kisha akamuambia Fatuma, mimi na wewe na hawa watoto wawili na huyu aliye lala (Ali) tutafufuliwa pamoja siku ya kiyama na tutakaa pamoja peponi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: Ewe Ali hatakupenda ispokua muumini na hata kuchukia ispokua mnafiki. Pia kuna hadithi inasema: Alama za mnafiki ni tatu: Anapo ongea hudanganya, akiahidi anahalifu, na akiaminiwa anafanya khiyana.

Mwisho napenda kuwaambia kua mimi ni mfuasi wa Ahlusunna waljamaa, nawashukuru sana wageni watukufu na wote mlio hudhuria na ninashukuru kualikwa kwetu na tunajivunia kuhudhuria katika kongamano hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: