Watu wa mji wa Lahlah Daru India: Ataba tukufu ni muendelezo wa juhudi njema za kuendeleza fikra na malengo ya Ahlulbait (a.s)…

Maoni katika picha
Shekh Nadhir Ahmadi Sharifu amebainisha kua Ataba tukufu zinafanya juhudi ya kuendeleza fikra na malengo ya Ahlulbait (a.s), na zinafanya kila ziwezalo kuhakikisha fikra na mtazamo wa Ahlulbait (a.s) unawafikia watu wote, kuwepo kwao pamoja na sisi leo hii ni uthibitisho wa ninayo sema, wametufanya tujihisi utukufu, hakika kusafiri kwao umbli mkubwa na kuvumilia kwao mateso ya safari ni kwa ajili ya kufikia lengo hilo tukufu, tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa moyo huu na kuhisi majukumu kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Aliyasema hayo katika ujumbe alio wasilisha kwa niaba ya wakazi wa mji wa Lahlah Daru kaskazini ya India, katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, lililo anza asubuhi ya leo Alkhamisi (18 Rajabu 1439h) sawa na (05 Aprili 2018m) katika hauza ya Ithna Ashariyya katika mji tajwa hapo juu.

Akaongeza kusema kua: “Mwenyezi Mungu mtukufu aliwajengea watu nyumba katika mji wa Maka, ambayo ni Kaaba tukufu uongofu na rehma kwa walimwengu, Kaaba tunaiita kua ni nyumba ya Mwenyezi Mungu, pamoja na kua hahitajii nyumba, kwani ametakasika na umbo, sisi ndio tunao hitaji nyumba ili itukinge kutokana na joto na baridi, lakini Mwenyezi Mungu mtukufu hana umbo la kuashiriwa ili ahitajie sehemu, sasa kwa nini imeitwa “nyumba ya Mwenyezi Mungu”. Uhai wa kila mtu unamtaka afanye ibada na ibada yeyote lazima iwe na kituo, Mwenyezi Mungu akajalia Kaaba kua ndio kituo cha watu, kila muislamu anaswali akielekea huko, kituo hicho kinahitaji mlinzi, na mlinzi lazima awe na madaraka ya ulinzi”.

Akaendelea kusema: “Mwenyezi Mungu akamteua Ali na akajaalia kuzaliwa kwake kuwe ndani ya Kaaba ili watu wote watambue kua Ali na watoto wake ndio walinzi wa kituo hiki na dini hii, kama alivyo sema Mtume (s.a.w.w): (Mfano wa Ali kwenu katika umma huu ni sawa na mfano wa Kaaba, kuiangalia ni Ibada na kwenda kuhiji ni faradhi)”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunawashukuru sana wageni wetu watukufu kwa kunawirisha macho yetu kutokana na kuangalia bendera za Ataba tukufu Husseiniyya, Abbasiyya na Askariyya katika maeneo ya miji yetu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: