Hauza ya Maimamu kumi na mbili yaswaliwa jamaa kubwa zaidi kwa sababu…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita linalo fanyika hivi sasa katika mti wa Karkal India, imeshuhudiwa swala ya jamaa kubwa zaidi, iliyo hudhuriwa na idadi kubwa sana ya watu walio jaa kwenye uwanja na katika ghorofa zote za jengo hilo na kila sehemu ya jemgo, sababu ya kujaa huko ni kutokana na kutambua kua imamu wa swala hiyo ndiye imamu wa swala katika haram ya Imamu Hussein (a.s), ambaye ni Sayyid Ibrahim Fadhil rais wa ujumbe wa Atabatu Husseiniyya tukufu unao shiriki katika kongamano hili, jambo hili ni tukufu sana kwao. Baada ya kumaliza swala Sayyid Ibrahim aliamua kumuelekea Mwenyezi Mungu na kuwaombea dua.

Kwa upande mwingine kama kawaida ya kongamano hili, ilisomwa dua Kumaili na msomaji wa Atabatu Askariyya tukufu bwana Qaiswar Swabaah Zuhair kwa sauti nzuri ya mahadhi ya kiiraq, ambapo wahudhuriaji waliisikiliza kwa heshima na unyenyekevu mkubwa.

Shekh Nadhir Mahdi Muhammadi kiongozi wa hauza ya Ithna Ashariyya alibainisha kua: “Hakika tangu kuanzishwa kwa hauza yetu tumesha swali mara nyingi swala zilizo hudhuriwa na watu wengi, lakini swala ya jamaa ya leo siku ya Alkhamisi ya mwezi mtukufu wa Rajabu katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtu bora baada ya Mtume (s.a.w.w) ambaye ni kamanda wa uislamu Imamu Ali (a.s), na Imamu wa swala hii ametoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, umati huu ulio shiriki swala hii haujawahi kutokea tangu kuanzishwa chuo hiki, hii yote inatokana na utukufu wa tunaye mkumbuka pamoja na juhudi kubwa zilizo fanywa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) hufanywa kwa ajili ya kuwaadhimisha Ahlulbait (a.s), pia ni sehemu ya juhudi ya kusambaza utamaduni, mwenendo na historia yao tukufu iliyo ifundisha dunia uislamu wa kweli, na kuonyesha utendaji wa Ataba tukufu za Iraq katika kuendesha makongamano, nadwa na mikutano ndani na nje ya nchi, kupitia shughuli hizo zinakua zimefungua milango ya kuwasiliana moja kwa moja na watu wa tabaka zote katika jamii na kuwafikishia ujumbe wa madhehebu sahihi, pia ni fursa ya kuelezea hatua za ujenzi na muundo wa uongozi wa Ataba tukufu, na vipi wamefanikiwa ndani ya muda mfupi kua vinara wa kupigiwa mfano mzuri katika kila sekta, kongamano hili limepitia hatua mbalimbali tangu kuanzishwa kwake hadi kufikia kuweka kituo chake mara hii katika mji wa Karkal India.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: