Dokta Mhakiki Mudharu Hiliy amesisitiza kua Atabatu Abbasiyya tukufu haijarudi nyuma katika kuhuisha turathi, kwa kufanya makongamano, nadwa na kutuma wataalamu wa fani hiyo katika kila kona ya Iraq kwenye maktaba za umma na binafsi kwa ajili ya kutafuta turathi, hayo aliyasema katika ujumbe wake alio toa katika hafla ya kufunga kongamano la “turathi zetu utambulisho wetu” kwa niaba ya wadau na wafadhili wa kuhuisha turathi, miongoni mwa aliyo sema ni:
Kila mtu anaye fuatilia turathi za umma huu anafahamu juhudi zinazo fanywa na Atabatu tukufu za hapa Iraq, katika harakati za kuhuisha turathi zikiongozwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya usimamizi wa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kissheria Sayyid Ahamadi Swafi, hakika Ataba hii haijarudi nyuma katika juhudi za kuhuisha turathi kwa kufanya makongamano, nadwa na kutuma wataalamu wake katika maktaba za Iraq za umma na binafsi kwa ajili ya kutafuta vitabu vya turathi.
Akaongeza kusema kua: “Ataba tukufu inatafuta kila kitabu, waraka au utafiti ulio andikwa na kila kitu kinacho weza kukusanywa kama turathi, kisha wakaamua kuanzisha vituo vya utafiti katika mji wa Karbala, Hilla na Basra, vituo hivyo vimefanya kazi kubwa katika sekta hii, vimekusanya nakala kale, vikazihakiki na vimehuisha turathi nyingi, na mji wa Hilla umeongoza katika hili, hakika Hilla ni mji ambao unavitabu elfu nne vilivyo andikwa Hilla, hilla ndio mji wa Allamah Hilliy na mhakiki Hilliy, na ibun Idrisa Hilliy, na Aali Twausi, hilla ni hazina kubwa ya turathi, Hilla ni moja ya mitazamo (madrasa) tatu za Fiqhi ya Jaafariyya, ambazo ni, madrasa ya Bagdad, madrasa ya Najafu na madrasa ya Hilla, lakini kwa hakika turathi zetu zimehodhiwa na nchi nyingi, hivyo Atabatu Abbasiyya haikutosheka na kutafuta turathi ndani ya maktaba za Iraq peke yake, bali imeenda pia katika maktaba za nchi zilizo hodhi turathi zetu kama vile, Ujerumani, Uingereza, Uturuki, Iran, Saudia na katika nchi zingine nyingi.
Akabainisha kua: “Hii ndio hali ya turathi zetu, na hizi ndio juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kukusanya turathi na kuzihuisha, Atabatu Abbasiyya tukufu ndio watu wa kwanza kufungua kituo cha turathi katika mji wa Hilla, na kituo hicho kinafanya kazi kama nyuki usiku na mchana, wanakusanya turathi sio za Iraq tu, bali wanatuma wataalamu wao hadi nje ya Iraq kwa ajili ya kukusanya nakala kale, na wanawasaidia wahakiki kila kona na wa viwango vyote wanao fanya uhakiki katika nakala kale hizo na kuzisambaza, nyingi zimekamilika na kazi bado inaendelea”.
Akafafanua kua: “kabla ya hapo tulikua tunapo taka kufanya uhakiki katika kitabu fulani cha nakala kale, tunapata tabu sana katika kuzipata nakala kale, miongoni mwa mambo ya lazima kwa mhakiki kama mnavyo fahamu, analazimika kukusanya nakala kale zote zinazo husiana na kitabu hicho, hapaswi kuacha nakala kale yeyote hata kama ikiwa mbali kiasi gani anatakiwa aifuate, kutokana na udhaifu wa hali ya muhakiki anaweza kushindwa kukusanya nakala kale nyingi na kujikuta anaanza kazi akiwa hana kitu, ndipo anasoma nakala kale moja kisha anaangalia nakala kale ipi muhimu na kuifanya kua msingi wa uhakiki wake, na nakala kale zingine zinakua ndio usaidizi wake, kisha anaprinti nakala kale hiyo katika program ya (Word), na anaendelea na kazi ya kuhakiki hadi mwisho, lakini hivi sasa unapo chagua maudhui tu, unavikuta tituo vya turathi vya Atabatu Abbasiyya tukufu tayali vimesha kuandalia kopi ya nakala kale na mada za kitabu na zipo tayali kwa kuprinti katika program ya (Word), inabaki kazi ya kuhakiki na kuprinti tu jambo ambalo ni rahisi sana katika uhakiki na kuhuisha turathi, baada ya Atabatu Abbasiyya tukufu kufungua kituo cha turathi katika mji wa Hilla, Atabatu Husseiniyya nayo ilishawishika na kufungua kituo cha Allamah Hilliy, vituo hivi vinafanya kazi kwa kushirikiana, hata kama vikifunguliwa vituo 100 vya kuhuisha turathi za Hilla havita tosha, kutokana na ukubwa wa jina la Hilla, watu wa Hilla na wanachuoni wa Hilla, tunatoa shukrani za dhati kwa Ataba zote za Iraq, hususan Atabatu Abbasiyya tukufu na kituo cha turathi za Hilla kutokana na kazi kubwa waliyo fanya ya kuhuisha turathi za Hilla na watu wote wa nyumba ya Mtume (a.s), na sisi kama wahakiki tupo tayali kutumia uwezo wetu wote kwa ajili ya kufanikisha kazi hii”.