Kila mtu anajua mafungamano yaliyopo kiitikadi na kihisia baina ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait na Maimamu wao (a.s), wanapo ona athari yeyote ya Imamu wao, nyoyo zao zinakua na hisia ya hali ya juu ambayo haielezeki, haya tumeyaona wazi pale yalipo funguliwa maonyesho ya vitu vinavyo tengenezwa na Ataba tukufu (Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya), zinazo shiriki katika kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, maonyesho yamewekwa katika matawi matati, kila tawi likiwakilisha Ataba, kuna aina mbalimbali ya bidhaa za vitengo vya habari na utamaduni, kama vile vitabu, majarida, vipeperushi, picha na vinginevyo, huku vitu hivyo vikiwa katika lugha ya kiingereza na kiurdu, vinavyo lenga watu wa tabaka zote, kuanzia mtoto hadi mzee.
Vile vile wameweka sanduku katika kila tawi kwa ajili ya kupokea barua zitakazo kusanywa baada ya kumaliza kongamano hili na kuzipelea katika madirisha ya makaburi kwa kila Ataba, pamoja na kugawa zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo hizo tukufu.
Rais wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao ndio wasimamizi wa kongamano hili, Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maonyesho ya vifaa vya kielimu na kitamaduni ni sehemu muhimu sana katika kongamano hili, tuliandaa vitu mbalimbali kwa ajili ya maonyesho haya, kwani yanafanyika kwa mara ya kwanza katika mji huu tena kwa mahudhurio makubwa kiasi hiki, tuliandaa sehemu maalimu katika maeneo ya hauza ya Ithna Ashariyya kwa ajili ya maonyesho, na tukachagua aina nzuri ya kufanya maonyesho, maonyesho haya ni fursa nzuri ya kuzielezea Ataba tukufu, kupitia machapisho au kwa kujibu maswali yanayo ulizwa na watu wanao kuja kuyatembelea, miongoni mwa mambo yaliyo wafurahisha zaidi ni kuwepo kwa bendera ya kila Ataba katika eneo lake kwa kiasi ambacho kila mtu anaweza kutabaruku nazo”.
Akaongeza kua: “Hakika maonyesho haya yanayo fanywa na matawi matatu ni sehemu ya muendelezo wa maonyesho kama haya yaliyo fanywa miaka ya nyuma, pamoja na kuzingatia mazingira ya kila mji yanako fanyikia, tumeongeza vitu vipya ambavyo havikuwepo katika maonyesho ya nyuma, tumechapisha maelfu ya nakala za vitabu na folda kwa lugha za kiengereza na kiurdu, machapisho yote yanamada nzuri na yamepambwa na picha za Ataba tukufu, pia tumetengeneza filamu za kiarabu, (zinazo elezea ushujaa wa Abulfadhil Abbasi a.s) na zimetengenezwa na idara ya picha zinazo cheza katika ofisi ya Intanet ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maonyesho yamepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa watu walio yatembelea, yamehudhuriwa na maelfu ya yatu walio kua na shauku ya kunufaika na maonyesho haya matukufu.