Hisia zisizo elezeka katika kundi la wafuasi na wapenzi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), angalia na ushuhudie jinsi macho yao yalivyo jaa hisia za mapenzi ya ardhi tukufu, wanatarajia ipo siku watanawirisha macho yao kwa kuangalia kubba ya malalo takatifu na kubusu kuta zake tukufu, haya yameonekana katika shughuli ya kupandisha bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) katika shule ya Imamu Khomeini kwenye mji wa Karkal India, tukio hilo ni miongoni mwa ratiba za kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita linano endelea katika mji tajwa hapo juu, na kuhudhuriwa na watu wengi sana, watu wamefurika katika uwanja wa shule na katika njia zinazo elekea katika shule hiyo tangu asubuhi, kwa nini isiwe hivyo wakati tukio hili ni kielelezo cha utukufu mwingi, ni kielelezo cha ushujaa, kujitolea na msimamo katika mwenendo wa Hussein.
Shughuli hii ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Askariyya bwana Qaiswar Swabaah, ukafuatia ujumbe wa Ataba tukufu zinazo shiriki katika kongamano (Husseiniyya, Abbasiyya na Askariyya) ulio wasilishwa na Sayyid Ibrahim Husseini, ambaye alisema kua: “Kwa hakika najiona mwenye bahati kubwa kusimama mbele yenu huku nyuso zenu zinawaka waka kutokana na nuru ya wilayah na nyoyo zenu zimejaa imani, bila shaka hafla hii ni majlis inayo mtaja Mwenyezi Mungu mtukufu na inaridhaa yake, imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: (kumtaja Ali ni ibada), kwa nini isiwe ibada wakati alizaliwa katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, na uhai wake wote amemtumikia Mwenyezi Mungu naye akampa kila kitu, Ali ni siri ya uwepo wa Mwenyezi Mungu na kwa kumtawalisha inapatikana radhi ya muabudiwa, kitu gani kitaniwezesha kuzungumzia utukufu wake wakati zama zimeshindwa kuleta mtu wa mfano wake”.
Akaongeza kua: “Hakika kufanya minasaba hii ni miongoni mwa mambo matukufu zaidi ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, hivyo Ataba tukufu za Iraq kwa kufuata maelekezo ya Marjaa dini mkuu, hufanya nadwa na makongamano pamoja na kuunda taasisi za kitamaduni kwa ajili ya kudumisha mawasiliano baina ya wapenzi wa Ahlulbait (a.s), kutokana na msingi huo ndio tumekuja kwenu kutoka katika nchi ya Iraq ya Ali na Hussein (a.s), ili tushirikiane na nyie katika furaha ya kukumbuka kuzaliwa kwa Imamu Ali (a.s) ambako bado tunaendelea kusherehekea hadi sasa”.
Baada ya hapo lilifuata tamko la ukaribisho lililo tolewa na Shekh Swadiq Rajaaiy, ambaye “Alitoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake kwa kuwapa zawadi ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo inamaana kubwa kwao, na akawashukuru wawakilishi wato wa Ataba tukufu walio shiriki katika shughuli hii, bendera hii itakua burudisho la macho ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), na itakua kielelezo cha amani na utulivu kwao, hakika Abbasi (a.s) ni mlango wa haja, ana heshima kubwa mbele ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.
Baada ya hapo wageni na wawakilishi wa taasisi mbalimbali wakaenda kupandisha bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakati ikipandishwa zilisikika sauti za wanao lia kwa furaha na wanao shangilia huku ikipepea katika anga la miji huu.
Shughuli hiyo ikahitimishwa kwa kusomwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa sauti ya msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Liith Abedi.
Baada ya hapo ugeni ulielekea katika shule nyingine ya kidini ambayo inaitwa shule ya Shahidi Mutwahari, baada ya mapokezi makubwa waliyo pewa na matamko ya ukaribisho kutoka kwa viongozi wa shule, Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri alizungumza kwaniaba ya wageni, alisema kua: “Tunawaunga mkono viongozi wa shule hii pamoja na walimu wote wa kiume na wakike, tunawaomba muendeleze juhudi hizi, hongereni sana kwa kazi nzuri”. Pia aliwahimiza wanafunzi wa kike washikamane na hijabu pamoja na misingi ya dini tukufu ya uislamu na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), ili wawe kielelezo cha msemo wa (Fatwimiyyaat) au (Zainabiyyaat), na akawahimiza wanafunzi wa kiume waongeze juhudi katika masomo, ili nao wawe kielelezo cha msemo wa (Husseiniyyin), wapambike na elimu kwa ajili ya kuitumikia dini ya kiislamu na madhehebu ya Ahlulbait (a.s)”.
Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukagawa zawadi kwa wanafunzi pamoja na walimu wao, kisha wakaagana kwa furaha kama walivyo pokewa na wakaondoka.