Miongozi kwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s): kugawa chakula kwa zaidi ya watu elfu kumi katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba yake Kiongozi wa Waumini (a.s)…

Maoni katika picha
Katika kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina linalo endelea hivi sasa katika miji wa Karkal India, ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu umegawa chakula kwa zaidi ya watu elfu kumi na tano, kama sehemu ya kutabaruku na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) katika sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba yake Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi Ustadh Saamir Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Wakazi wa mji wa Karkal wana mapenzi maalumu kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), na wana mafungamano makubwa na Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuhakikisha wanatabaruku katika baraka zake, tumepika chakula cha watu elfu kumi na tao, kwa ajili ya kukigawa katika hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali (a.s) miongoni mwa ratiba za kongamano hilo”.

Akaongeza kusema kua: “Chakula hicho kimepikwa kwa ushirikiano na wapishi wa mji huu, kiliwekwa katika vifungashio maalumu na kugawiwa katika ufunguzi wa kongamano, watu walihudhuria kwa wingi sana kwa ajili ya kufuata baraka ya chakula hicho cha mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s)”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) hufanywa kwa ajili ya kuwaadhimisha Ahlulbait (a.s), pia ni sehemu ya juhudi ya kusambaza utamaduni, mwenendo na historia yao tukufu iliyo ifundisha dunia uislamu wa kweli, na kuonyesha utendaji wa Ataba tukufu za Iraq katika kuendesha makongamano, nadwa na mikutano ndani na nje ya nchi, kupitia shughuli hizo zinakua zimefungua milango ya kuwasiliana moja kwa moja na watu wa tabaka zote katika jamii na kuwafikishia ujumbe wa madhehebu sahihi, pia ni fursa ya kuelezea hatua za ujenzi na muundo wa uongozi wa Ataba tukufu, na vipi wamefanikiwa ndani ya muda mfupi kua vinara wa kupigiwa mfano mzuri katika kila sekta, kongamano hili limepitia hatua mbalimbali tangu kuanzishwa kwake hadi kufikia kuweka kituo chake mara hii katika mji wa Karkal India.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: