Macho yalilia kwa kuwekwa kwake na watu wamefanya matembezi ya kimbunga: Waumini wa Karkal wanapokea bendera za kubba za Ataba tukufu za Iraq…

Maoni katika picha
Ilipo fika asubuhi ya siku ya Alkhamisi (18 Rajabu 1439h) sawa na (5 Aprili 2018m), ambayo ndio siku ya kuanza kwa kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-minina (a.s) la mwaka wa sita katika mji wa Karkal India, ambalo katika ratiba yake ya ufunguzi kuna kipengele cha kupandisha bendera za kubba za malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi pamoja na Maimamu wawili wa Askariyyaini (a.s), watu walimiminika kwa wingi kuja kuangalia upandishwaji wa bendera hizo, pamoja na baridi kali lililopo na hali ya hewa ngumu inayo badirika badirika lakini watu hao walifika mapema sana ya asubuhi.

Kutokana na kufanyika kwa kongamano hili pamoja na shughuli ya kupandisha bendera inayo fanyika kwa mara ya kwanza katika kiwango hiki hapa katika mji wa watu masikini kiuchumi matajiri kiroho wenye mapenzi ya kweli kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), kazi zote za mji huu zimesimamishwa, maduka yamefungwa na shule zime simama kwa ajili ya kutoa nafasi kwa watu ya kuja kuhudhuria katika kongamano hili, na kunawirisha macho kwa kuangalia upandishwaji wa bendera za Ataba tukufu za Iraq, hivyo watu walifurika sana katika shule ya Ithna Ashariyya na barabara zinazo elekea katika shule hiyo unako fanyika ufunguzi wa kongamano hili, ambalo ni tukio kubwa sana kwao, watu kutoka katika vitongoji jirani pia walihudhuria, kwa ufupi mahudhurio yalikua ni makubwa sana tunaweza kusema watu walikua ni makumi ya maelfu.

Watu wametembea umbali mkubwa hadi kufika katika hauza ya Ithna Ashariyya sehemu zinapo pandiswa pendera hizo, shughuli ya kupandisha bendera ilipo anza watu walishangilia sana na mazingira yalikua kama ya Ashura au Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), huku wengine wakitokwa machozi na wakisema (Labbaika yaa Hussein) na (Abadan Wallahi yaa Zaharaa laa nansa Husseinaa) na (Haihaata minna dhilla) kwa kweli mazingira yalikua kana kwamba bendera za Kubba zimekuja kuzindua msimu wa Ashura au Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Hakika hatuoni maneno yanayo faa kuelezea mazingira halisi yalivyo kua.. kushindwa huku ni jambo la kawaida hususan itakapo kua jambo linahusu kuelezea utukufu na sifa.. na hapa namaanisha hakuna anaye weza kumuelezea kwa ukamilifu Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Maimamu wawili wa Askariyyaini (a.s).

Kamera ya Alkafeel ilikuwepo na inakuleteeni picha chache za tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: