Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Hakika ulinganisho kati ya turathi zetu za kiarabu na kiislamu na nakala kale za kimataifa hakina uwiyano unao ridhisha.

Maoni katika picha
Iwapo mfatiliaji wa mambo ya turathi akifanya ulinganisho wa haraka haraka baina ya turathi zetu za kiarabu na kiislamu na turathi za kimataifa, atakuta hakuna uwiano unao ridhisha, inasemekana kua; kuna nakala kale nyingi katika maktaba za kimataifa, hususan maktaba za Uingereza katika jiji la Landan inakadiriwa kua kuna nakala kale elfu (15) na karibu nakala kale elfu (55) zipo China na katika nchi zingine kama vile Iran, Uturuki na nchi zingine.

Haya yamesemwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar katika ufunguzi wa mkutano wa (Siku ya nakala kale za kiarabu) unao simamiwa na Maktaba kwa kushirikiana na Daru Makhtutwaat Al-arabiyya, chini ya Umoja wa nchi za kiarabu Kairo, na kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu cha chuo kikuu cha Bagdad, chini ya kauli mbiu isemayo (Quds, Turathi zinapo kua mateka), katika ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), asubuhi ya leo Juma Mosi (20 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m).

Yafuatayo ni mambo muhimu aliyo ongea katika ujumbe wake

Kudhihiri kwa uislamu kulileta mabadiliko makubwa katika kila sekta za uhai wa jamii katika nchi za kiarabu, kisha mabadiliko hayo yakaenea katika jamii zote, na yalikua chini ya tawala za kiarabu na kiislamu, sekta ya elimu na utamaduni ni miongoni mwa sekta muhimu zilizo pata mabadiliko, uislamu ulikua unawataka wafanye tafakuri, kwa ajili ya kutunza elimu na kuwapa heshima wanachuoni, mabadiliko yalifikia malengo, kama vile katika elimu za Qur’an, hadithi za Mtume mtukufu, elimu za lugha ya kiarabu, pamoja na elimu ya swarafu, na katika kila sekta ya kielimu, kulikua na watu walio fanya kazi ya kusambaza elimu, wakaeneza wanafunzi wao kila mji, kisha wakaandika vitabu na kutuachia urithi ambao unaendelea kuongezeka mwongo baada ya mwongo na karne baada ya karne, hadi umma wa kiarabu na kiislamu ukazidu umma zingine, pamoja na ada mbalimbali zilizopo, turathi zilizo tufikia ni nyingi sana, kazi ya kuzisambaza inahitaji ushirikiano, iwapo mtafiti akifuatilia na akalinganisha kwa haraka haraka baina ya turathi zetu za kiarabu na kiislamu na nakala kale za kimataifa atafahamu kua hakuna uwiano baina yake, inasemekana kua kuna nakala kale nyingi katika maktaba za kimataifa, hususan maktaba za Uingereza katika jiji la Landan inakadiriwa kua kuna nakala kale elfu (15) na karibu nakala kale elfu (55) zipo China na katika nchi zingine kama vile Iran, Uturuki na nchi zingine.

Akaoneza kusema kua: “Kuzilinda na kuzisambaza kunahitaji juhudi za pamoja, pamoja kua nchi nyingi za kiarabu zimelipa umuhimu swala la turathi na nakala kale kwa kuanzisha taasisi mbalimbali za turathi zenye jukumu la kuzihuisha na kuzisambaza na kazi kubwa inayo fanywa na taasisi hizo, lakini pamoja na hatua hizo zilizo fanywa na nchi za kiarabu bado hazitoshi, kulingana na hazina ya turathi iliyopo katika umma wa kiarabu na kiislamu, hivyo tunahitaji kufanya makongamano na mikutano kama hii kwa ajili ya kuhimiza kuhusu turathi za nakala kale, kuzihimiza taasisi za turathi katika nchi zote za kiarabu ziongeze juhudi za kuhuisha kilicho bakia katika turathi”.

Akabainisha kua: “Hii juhudi tukufu iliyo fanywa na Maahadi ya nakala kale za kiarabu ya kuteua siku maalumu ya turathi za kiarabu ni muhimu sana, kwa ajili ya kuvitambulisha vizazi vijavyo turathi zao zilizo andikwa na nafasi yake katika kustaarabisha mataifa mengine, hali kadhalika kuzihimiza taasisi za turathi za kiarabu na kiislamu wazifanyie kazi turathi zetu zilizo bakia, na kuzirudishia uhai wa kihistoria na kuzitoa katika mwanga, pamoja na kulinda misingi muhimu”.

Akafafanua kua: “Hapa Iraq zimejitokeza taasisi za turathi ambazo zimefanya vizuri katika sekta hii, kama vile kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu kilicho chini ya chuo kikuu cha Bagdad, na vinginevyo katika vituo rasmi na visivyo kua rasmi, mfano wa kinacho fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, kuhusu kuzienzi turathi za kiislamu, tulianza kukusanya turathi zilizo kua zimetapakaa na zilizo sahaulika, na leo hii tumesha unda kituo rasmi kinacho fanya kazi hiyo, ushirikiano wetu na Maahadi ya nakala kale za kiarabu ya Kairo pamoja na kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu cha chuo kikuu cha Bagdad katika mkutano huu, ni miongoni mwa matunda ya namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyo jali sekta hii, kwa hakika tunawashukuru sana wote mlio hudhuria, tunawakumbusha kazi kubwa inayo fanywa na wanajeshi wetu na Hashdi Sha’abi ya kulinda taifa hili, hakika wao wanastahiki zaidi kushukuriwa kwa kulinda amani na utulivu wa taifa hili pamoja na kuhifadhi urithi na maeneo matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: