Chini ya kauli mbiu: (Quds, turathi zanapo tekwa), kuanza kwa mkutano wa siku wa nakala kale za kiarabu unao simamiwa na ofisi ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na Maahadi ya nakala kale za kiarabu ya umoja wa nchi za kiarabu.

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Juma Mosi (20 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m) ofisi ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza program za ( siku ya nakala kale za kiarabu) kwa kushirikiana na Maahadi ya nakala kale za kiarabu chini ya umoja wa nchi za kiarabu wa Kairo pamoja na kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu cha chuo kikuu cha Bagdad chini ya kauli mbiu isemayo: (Quds, turathi zinapo tekwa), katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar.

Kisha ukafuata ujumbe wa Maahadi ya nakala kale za kiarabu wa umoja wa nchi za kiarabu wa Kairo, ulio wasilishwa na mkuu wa Maahadi hiyo Dokta Faisal Fiyaan ambaye amesima kua: Siku ya nakala kale za kiarabu awamu ya sita, kwa hakika ni tukio kubwa la kitamaduni, Atabatu Abbasiyya ilishirikiana nasi mara ya mwisho na ushiriki wao ulikua muhimu sana, pia tunashirikiana katika siku ya nakala kale za kiarabu ya mwaka huu, chini ya kauli mbiu (Quds…turathi zinapo tekwa), tunatambua kua kutekwa kwa turathi katika nchi ya Palestina kulianza tangu karne iliyo pita na zimeendelea kutekwa hadi leo, bado turathi za nchi hiyo zimetekwa, kutekwa ni kitendo cha kumuweka mtu chini ya udhibiti, anaweza kua kafungwa mikono na miguu, lakini kutekwa kubaya zaidi ni kutekwa kwa akili ya mwanadamu na fikra zake, leo kuna turathi nyingi sana hapa duniani, mamilioni ya nakala kale yamesambaa kila sehemu ya dunia, watu wengine wanazitambua na kuzikubali lakini sisi wahusika wakuu hatuzitambui.

Akaongeza kusema: “Tuna haki zaidi ya kuzihifadhi, kuzihifadhi kwake sio kwa kuzijua juu juu, inatakiwa tuzifahamu kwa undani, utambuzi utakao tuwezesha kuzilinda, sio kwa kuziweka katika shelfu za maktaba peke yake, bali inatakuwa kuzihuisha na kunufaika nazo, swala la turathi leo hii linatakiwa kua sehemu muhimu katika jamii za waarabu, utamaduni wetu wa leo hauwezi kupata sura katika zama hizi za utandawazi ispokua kwa kupitia turathi zetu, kwa sababu turathi ndio zinazo tutambulisha, tunajiuliza kwa nini leo tunahitaji idadi kubwa ya watu watakao fanya uhakiki wa turathi zetu na kutuweka nazo karibu, pia yatupasa kujiuliza uhakika wa kazi zao, tunafikiria kua tupo katika dunia tunayo weza kuiita kua (dunia ya nakala), sasa tunatakiwa kuingia hatua ya pili ambayo ni dunia ya kunufaika na nakala hizo, huku turathi zetu zikiwa zimetekwa, sio kwamba zimetekwa nakala za maandishi tu, bali umetekwa hadi uwelewa wa nakala kale, uwelewa na akili ni sehemu ya miili yetu, mara nyingi mimi husema haifai kutenganisha baina ya mwanadamu na turathi, hakika mwanadamu ndio turathi.

Akabainisha kua: “Utekwaji wa turathi ni tatizo la ujumla, linatakiwa kuzungumzwa hususan tunapo fanya hafla kwa ajili ya nukta hiyo, na kuhusu namna ya kunufaika nazo, utatuzi wake upo kwetu na katika historia yetu na tamaduni zetu, utatuzi wenyewe sio wa kinadhariya peke yake, turathi hizi zinamilikiwa katika maktaba, vyuo vikuu na katika taasisi za kielimu hususan za Waisraeel, hivyo utatuzi lazima uambatane na vitendo vya kuzisafisha turathi zilizo chafuliwa kwa kuishi mbali nasisi kwa muda mrefu.

Ukafuata ujumbe wa kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu wa chuo kikuu cha Bagdad, ulio wasilishwa na mkuu wa kituo Dokta Majidi Mukhlif ambaye amesema kua: “Ni furaha kubwa kuona kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu cha chuo kikuu cha Bagdad ni moja ya walio changia kufanikisha kwa hafla hii tukufu ambayo imekua ikifanywa na nchi za umoja wa kiarabu, pia ni furaha kubwa kwangu kumuwakilisha rais wa chuo kikuu cha Bagdad Dokta Alaa Abdulhussein katika hafla hii, na kukufikishieni salamu zake, anapongeza sana hafla hii na anaomba ushirikiano huu uendelee baina ya chuo kikuu cha Bagdad kupitia kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu pamoja na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ndugu zangu watukufu, hakika turathi zetu ni nyingi sana tunayazidi mataifa mengine, yatosha kuona kua anuaji (majina) yake tu yapo katika mamia ya kurasa, bali ni malaki kama sio mamilioni ya nakala kale, hivyo lazima kujivunia turathi za umma wetu wa kiarabu na kiislamu, haitoshi kuzitambulisha kwa wanadamu peke yake bali inatakiwa tuweze kunufaika na kila kipengele katika kujenga jamii mpya ya kiislamu yenye maendeleo, kuzienzi na kuzifanyia kazi turathi zetu sio kurudi nyuma kama wanavyo sema baadhi ya watu, bali ni siraha ya kutupeleka mbele kwenye maendeleo, kwani turathi zetu ndio msingi wetu lazima tuzitumie kusonga mbele hatuwezi kujitenga na mambo yetu ya zamani, hivyo lazima tusonge mbele kwa kutumia turathi zetu, na tuzioanishe na zama zetu za sasa kwa kutambue vyema wakati ulio pita, tunaweza kujenga wakati ujao wenye mafanikio na maendeleo, leo tunafanya hafla ya siku ya nakala kale za kiarabu ndani sehemu hii tukufu, yatupasa kukumbuka kua siku ya nakala kale ni siku muhimu sana kwa maslahi ya umma, tunatakiwa kuwajibika katika kuhakikisha tunazitunza nakala kale za kiarabu na kiislamu na kuzihuisha sambamba na kuziboresha, hii ni vita ya kijamii na kitamaduni, siraha yake ni kurejea katika turathi sahihi, hatukanushi juhudi zinazo fanywa na Maahadi ya nakala kale na nafasi yake katika kuzihudumikia turathi, kwa kufanya vikao mbalimbali vya kielimu na kuondoa pazia katika turathi tofauti kila pembe ya dunia, chini ya misingi ya kielimu, na ushiriki wa vituo vya usambazaji katika kufichua nakala kale za kielimu, kimaadili au kihistoria”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: