Kumalizika kwa kongamano la siku ya nakala kale za kiarabau, kamati ya maandalizi yaweka maazimio kadhaa…

Maoni katika picha
Chini ya anuani: (Quds, turathi zanapo tekwa) Alasiri ya Juma Mosi (20 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m) kikao cha siku ya nakala kale za kiarabu kilicho simamiwa na ofisi ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na Maahadi ya nakala kale za kiarabu ya umoja wa nchi za kiarabu wa Kairo pamoja na kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu cha chuo kikuu cha Bagdad kilihitimishwa.

Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi, na maelezo ya mwisho yalitolewa na Ustadh Muhammad Muhammad Hassan ambaye ni mwakilishi wa mkuu wa kituo cha kuhuosha turathi kilicho chini ya ofisi ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, alisema kua:

Hakika miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwetu, ametuwezesha kukumbuka umuhimu wa turathi za umma wetu wa kiarabu na kiislamu, hazina kubwa ya karatasi na vitabu imeandikwa na wanachuoni na watafiti wetu ambayo imekua kimbilio la kila mpenzi wa elimu.

Akaongeza kusema kua: Ndio! Turathi za umma wa kiislamu zina misingi imara iliyo jenga mustaqbali wake kutokana na wakati wa sasa na ulio pita, zimeweza kuhuisha umma na mataifa kwa kuzitaja na kuzungumza historia yake, zimekua ndimi faswaha na dhamira za kweli, bali zimekua na upekee mkubwa, zina umri wa karne na karne, hazija haribiwa na maadui, zimeendelea kufanyiwa njama na vituko vingi katika historia yake, pamoja na hivyo zimeendelea kua imara na kupendwa na watu wake katika kila zama.

Akasema: Leo hii turathi hizi zimetujia zikiwa na majeruhi, na kutupa jukumu la kuzilinda na kuzihami kutokana na maadui wanaotaka kufuta utambulisho wa kiarabu na kiislamu, hebu tunyooshe mikono yetu na tushirikiane kutibu majeraha hayo na tuzilinde, sitaki kurefusha maneno ndugu zangu watukufu, lakini tunafahamu kua katika vifua vya wapenzi kuna maumivu makubwa, kutokana na matatizo yanayo zikumba turathi hizi tukufu, yaliyo tokea Iraq na Sirya katika miaka ya hivi karibuni, na yale yaliyo tokea Palestina miaka ya nyuma pamoja na katika miji mingine ya kiislamu ya kuibwa na kuchomwa turathi za kiislamu ni mfano wa wazi wa nilicho kisema.

Akabainisha kua: Kinacho tia moyo ni kuona kuna watu wamejitolea kuzilinda turathi na nakala kale, na wamepiga hatua kubwa katika hilo, na miongoni mwa juhudi zao ni kufanyika kwa hafla ya siku ya nakala kale za kiarabu, ambayo mwaka huu imesimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ofisi ya Daru Makhtutwaat na kwa kushirikiana na Maahadi ya nakala kale za kiarabu ya Kairo pamoja na kituo cha kuhuisha turathi za kiarabu na kiislamu cha chuo kikuu cha Bagdad, ikiwa ni safari ya utendaji wa pamoja unao takiwa kufanywa na taasisi tofauti, ili wawe na kauli moja na msimamo mmoja dhitu ya turathi zao tukufu, na kuchagua kauli mbiu isemayo, Quds, turathi zanapo tekwa, ili kuamsha hisia za kulinda turathi zetu na nakala kale.

Tumependa tusiondoke hapa bila kua na maazimio yatakayo changia katika kulinda turathi zetu na kuzihuisha, maazimio tuliyo andika ni haya yafuatayo:

Kwanza: Kuzitambulisha turathi zetu na nakala kale za kiarabu na kiislamu katika taasisi za kijamii, katika tabaka tofauti kuanzia wazee hadi vijana, ili watu wote watambue umuhimu wa turathi hizo kwao, utamaduni wa kuzithamini nakala kale uenee katika jamii nzima.

Pili: Umuhimu wa kusaidiana na kuwasiliana kwa (taasisi na watu) wanao fanya utafiti katika sekta hii kwa ajili ya kuzihifadhi na kuzihuisha.

Tatu: Umuhimu wa kubadilishana maarifa na kusaidiana kwa (taasisi na watu) katika kuandika faharasi za turathi na nakala kale na kuziwasilisha kwa wahakiki na watafiti kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao.

Nne: Umuhimu wa kuanzisha Maahadi za kisekula kwa ajili ya kufundisha elimu ya uhakiki wa nakala kale na faharasi pamoja na ukarabati wake kwa mujibu wa selebasi za kimasomo za kisasa, na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu ichukue nafasi yake katika sekta hii.

Katika jambo hili, Atabatu Abbasiyya tukufu tangu miaka miwili iliyo pita, baada ya kupewa baraka na kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, walianza mradi wa kufungua Maahadi ya kisekula ya watu walio bobea katika sekta ya turathi na nakala kale (uhakiki, faharasi na ukarabati), wamesha piga hatua kubwa katika kufuatilia swala hilo pamoja na vikwazo vilivyo jitokeza vya kanuni kutokana na jina lenyewe la (turathi na nakala kale) na bado wanaendelea na mchakato wa kufikia katika lengo.

Tano: Umuhimu wa kushirikiana na kuunda kanuni za pamoja kuhusu sifa za faharasi za nakala kale zote zilizo hifadhiwa katika mikoa yetu mitukufu na katika maktaba zetu, maslahi ya umma lazima yaheshimiwe kuliko maslahi binafsi.

Sita: Umuhimu wa kuwasiliana kwa vituo vya uhakiki, na kutambulishana nakala zilizo hakikiwa, ili kuepuka kujirudia rudia kusiko kua kwa lazima, kuwasiliana huko pia kutasaidia kuongeza idadi ya uhakiki wa turathi na nakala kale zetu.

Saba: Umuhimu wa kufanya nadwa, mikutano na makongamano kuhusu turathi na nakala kale katika sekta maalumu kwa ajili ya kuzitambulisha na kubadilishana uzowefu jambo litakalo leta maendeleo katika sekta hii.

Mwisho wa kikao vikatolewa vyeti kwa washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: