Ataba tukufu zafanya mahafali za usomaji wa Qur’an katika mji wa Karkal na wakazi wa mji huo waisikiliza kwa unyenyekevu…

Sehemu ya mahafali katika mji wa Sanko
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, linalo endelea sasa hivi katika mji wa Karkal kaskazini ya India katika ratiba yao wameweka kipengele cha usomaji wa Qur’an tukufu, sauti ya Mwenyezi Mungu ambayo huingia katika nafsi ya mtu na kuamsha hisia zake pindi anapo isikiliza kwa mazingatio, hivyo vimefanyika vikao vya usomaji wa Qur’an kwa ushiriki wa wasomaji wa Ataba tukufu za Husseiniyya, Abbasiyya na Askariyya, kipengele hicho kimeongeza hadhi na utukufu wa kongamano.

Waumini wa mji huu wanaheshimu sana usikilizaji wa Qur’an, hali itakua vipi atakapo kua msomaji anatoka katika ardhi takatifu tena katika Ataba tukufu, kikao cha kwanza cha usomaji wa Qur’an kilifanyika katika Muswalaya Mahdiyya kwenye kitongoji cha Sanko kilichopo katika jimbo ja Karkal, usomaji hua ulianza baada ya kupandishwa bendera za Maimamu wawili wa Askariyyaini (a.s), na alishiriki msomaji wa Atabatu Husseiniyya tukufu Falaah Zaliif na bwana Leeth Abedi kutoka katika Atabatu Abbasiyya na Quswair Swabaah kutoka katika Atabatu Askariyya tukufu, waliburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa usomaji wa mahadhi tofauti na kwa sauti nzuri.

Kikao kingine cha usomaji wa Qur’an kilifanyika walipo tembelea shule ya Jaafariyya, na walisoma walewale wageni kutoka katika Ataba tukufu walio waburudisha wahudhuriaji kutokana na uzuri wa sauti zao na mahadhi ya usomaji wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: