Imamu Ali (a.s) alikua karibu sana na mayatima ndio maana akapewa jina la baba wa mayatima (Abul Aitaam) hakika alikua na uhusiano mkubwa na mayatima kiasi kwamba hauwezi kumtenganisha nao, bila shaka sifa hiyo tukufu walikua nayo pia watoto wake watakatifu (a.s), hivyo kamati ya maandalizi ya kongamano la Amirul Mu-minina (a.s), haikutaka kukosa kipengele cha kuonyesha kuwajali mayatima katika ratiba ya kongamano linalo endelea hivi sasa katika mji wa Karkal, kwa kutembelea taasisi zinazo lea mayatima, kwani kufanya hivyo kunawajenga kisaikolojia na kuacha athari kubwa katika nafsi zao.
Ugeni ulitembelea shule ya Jawaadiyya Alkhairiyya, ambayo ni taasisi ya kielimu na kimalezi ya kidini inayo toa huduma za kimalezi na kielimu kwa mayatima, baada ya kukutana na viongozi wa taasisi hiyo, mkuu wa taasisi hiyo Shekh Muhammad Baaqir alitoa tamko la ukaribisho, ambapo alitoa shukrani nyingi kwa kutembelewa na ugeni ambao hajawahi kupokea ugeni kama huo, hii inamaanisha umuhimu na heshima kubwa ya Ataba tukufu za Iraq kwa kundi hili la mayatima, pamoja na hivyo wanafunzi hao wamefanya vizuri katika masomo yao, wamefaulu kwa daraja za juu na kuingia katika vyuo vikuu kwenye michepuo tofauti.
Kisha ukafuata ujumbe wa wageni ulio wasilishwa na Sayyid Ihsaani Gharifi, alionyesha kufurahishwa kwa wageni kutokana na juhudi nzuri za wanafunzi hawa ambao wanapambana na hali ya uyatima na wameishinda kwa kufaulu katika masomo yao na kuendelea na elimu ya juu.
Wanafunzi walio kuwa wanapewa zawadi pia walikua na ujumbe ulio wasilishwa na mwanafunzi Shaukat Ali, nao pia walitoa shukrani nyingi kwa ugeni huu na kusema kua umewapa msukumo mkubwa wa kuendelea na masomo.
Rais wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri alielezea furaha waliyo nayo wageni hususan baada ya kuona mabinti wenye maisha magumu likiwemo la uyatima ndio walio shika nafasi za kwanza na akawahimiza wenzao kuiga mfano huo, akawahimiza wote kwa pamoja waongeze juhudi ya kutafuta elimu na wamfanye Mtume (s.a.w.w) kua kigezo chao.
Kituo cha pili walitembelea taasisi ya Zaharaa (a.s) ya kulea mayatima wa kike, ambayo ipo chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, na inazaidi ya mayatima (50), taasisi inawagharamia kila kitu, maisha, masomo na vinginevyo kwa ajili ya kuwaandaa kua wanawake watakao weza kubeba majukumu.
Katika tamko la ukaribisho rais wa kamati kuu ya uongozi wa taasisi hiyo Shekh Ridhwa Ridhwani aliwashukuru wageni kwa kusafiri umbali mkubwa kwa ajili ya kuja kuitembelea taasisi hii, akasema kua taasisi hii imeanzishwa mwaka (2004) chini ya ufadhili wa Marjaa dini mkuu, muda wa masomo ni miaka (12) wanaanza hatua ya awali hadi sekondari, miongoni mwao wapo waliofika elimu za juu.
Mjumbe wa kamati inayo simamia taasisi hii Profesa Naadhir Shabani alifafanua selebasi wanayo tumia katika masomo, na akamalizia kwa kushukuru ziara hii, akasema anaomba itokee tena siku za mbele, akasisitiza kua ugeni huu utawapa msukumo mkubwa walimu na wanafunzi katika kutekeleza majukumu yao bila kuhisi uyatima wowote.
Mwisho kabisa wageni nao wakazungumza neno lao lililo wasilishwa na Sayyid Ihsaani Gharifi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ammaye alitoa shukrani kwa viongozi wa taasisi hii kuanzia kamati kuu ya uongozi na walimu, kutokana na kazi wanayo fanya ya kuwalea mayatima na kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida na kuchanganyika na makundi mengine ya jamii.
Baada ya hapo mayatima wakapewa zawadi pamoja na walimu wao huku wakishangilia sana na kuwaahidi wageni kua wataendelea kutekeleza mradi huu wa kibinadamu.