Ugeni wa Ataba tukufu za (Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) uliopo katika mji wa Karkal India, kushiriki katika kongamano la kitamaduni Amirul Mu-minina (a.s) la mwaka wa sita, umeshiriki katika kuweka jiwe la msingi wa chuo cha Albatuul cha mayatima wa kike katika mji huo, ambacho kinatarajiwa kupokea mayatima wa kike na kuwafundisha masomo ya kisekula na kidini kwa kufuata selebasi maalimu itakayo waondolea unyonge wa uyatima walio nao.
Jambo hili ni la kwanza hapa india hususan katika mji wa Karkal, nalo ni miongoni mwa miradi iliyo chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani, walichelewesha kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuusubiri ugeni huu ili waweze kupata baraka zao, pia wameweka baadhi ya vitu vya kutabaruku zikiwemo turba za Imamu Hussein (a.s) katika msingi huo, ujenzi wa chuo hicho ni alama ya kihistoria kua watumishi wa Ataba tukufu za Iraq waliwahi kufika hapa.
Wasimamizi wa mradi huu wamefurahishwa sana na jambo hili na wameahidi kufanya kazi kwa bidii, chuo hiki kinajengwa katika uwanja wenye ukubwa wa (mita 702) kwa kufuata ramani ya jengo linalo endana na mazingira ya kimasomo.
Tukio hili lilikamilishwa kwa kusoma Duaau Faraji ya Imamu Swahibu Zamaan (a.f) kisha wageni wakaagwa kwa furaha kama walivyo pokelewa.