Ugeni unao wakilisha Ataba tukufu za Iraq waitembelea shule ya Jaafariyya na taasisi ya Ridhwa ya kidaktari na kihandisi…

Maoni katika picha
Shule ya Jaafariyya ni moja ya shule kubwa za kidini na kisekula katika mji wa Karkal India, na inafungamana na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu, miongoni mwa ratiba ya kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-minina (a.s) la mwaka wa sita kulikua na kipengele cha kutembelea shule mbalimbali na kuangalia selebasi za masomo pamoja na kutoa zawadi za tabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ugeni ulipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa wanafunzi na walimu wao, kisha wakasikiliza tamko la ukaribisho kutoka kwa Shekh Sayyid Adhafari aliye zungumza kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo, alitoa shukrani za dhati kwa kutembelewa na ugeni huo, unao toka katika ardhi tukufu na maeneo matakatifu nchini Iraq, akasema kua ziara hii ni ya kihistoria katika shule hiyo kwani hawajawahi kupokea ugeni kama huu tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka (1995m), akafafanua kua hii ni taasisi ya elimu ya dini na sekula, inawanafunzi zaidi ya (550) kuanzia kiwango cha awali hadi sekondani, wamekua wakifaulisha vizuri kwa mujibu wa viwango vya mji huu pamoja na kua na vifaa duni, jitihada za wanafunzi katika masomo zinazo tokana na mapenzi yao kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) ndio siraha kubwa inayo fanya wafaulu.

Mkuu wa shule Sayyid Ali pia aliwashukuru wageni kwa kutumia maneno matamu zaidi ya ukaribishaji, akasema kua hawajawahi kupata ugeni mkubwa kama huu ulio kuja kuwatia moyo wao na wanafunzi wao kama hivi, walio vumilia tabu ya safari ndefu kwa ajili yao, shukrani zetu kwenu zinatoka ndani ya nyoyo zetu, na tunawaomba mtukumbuke daima katika dua zenu.

Kikafanyika kikao cha usomaji wa Qur’an kilicho ongozwa na wasomaji kutoka katika Ataba tukufu za Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya, baada ya hapo wageni wakaenda kutembelea taasisi ya Ridhwa (a.s) ya kidaktari na kihandisi, nayo inafungamana na Marjaa dini mkuu vile vile, inatoa huduma mbalimbali za kibinadamu ikiwemo matibabu, na huduma zote inatoa bure, viongozi wa taasisi hiyo waliushukuru sana ugeni kwa kuwatembelea, nao wageni waliwahimiza kuendelea kuwahudumia wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wa mji huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: