Wanachuoni wa Karkal: Imechomoza alfajiri katika ardhi yetu kwa kupepea bendera za kubba za malalo ya Maimamu (a.s) huu ni utukufu mkubwa kwetu hakika tunafuraha isiyo kifani…

Maoni katika picha
Katika kikao kilicha wahusisha wageni kutoka katika Ataba tukufu za Iraq (Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) na jopo kubwa la wanachuoni na wanafunzi wa hauza ya Ithna Ashariyya katika mji wa Karkal India, ikiwa ni miongoni mwa ratiba za kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, wanachuoni hao, walitoa ujumbe ulio wasilishwa na Sayyid Mahdi Mussawi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tumepokea wageni kutoka katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi pamoja na haram ya Maimamu wawili ya Askariyyaini (a.s), karibuni sana wageni wetu kutoka katika ardhi ya Iraq, ardhi ya Ali na Hussein (a.s), mmetufurahisha sana, hakika mmeingiza furaha katika kila nyumba ya Karkal, na kilicho ongeza furaha zaidi ni kuja kwenu na bendera za kubba ya Imamu Hussein, Abbasi na Askariyyaini (a.s), ambazo baada ya kupandishwa katika mji huu imechomoza alfajiri mpya ambayo haikuwahi kuchomoza siku za nyuma, mmetufanya tujivune kwa watu wengine kutokana na utukufu huu, tunawashukuru sana kwa kuchagua kwenu kuja katika mji huu wenye mapenzi na Ahlulbait (a.s), mmesafiri umbali mkubwa hadi kufika huku kaskazini ya India, Mwenyezi Mungu awalipe heri nyingi na aliweke hili katika mizani ya matendo yenu, tunatarajia mrudi tena miaka ya ijayo, mmepata taufiq ya kushikamana na kitu kikubwa pamoja na kuadhimisha alama za Mwenyezi Mungu”.

Kisha wageni kutoka katika Ataba tukufu wakachangia mazungumzo hayo, akaanza Sayyid Ibrahim Husseini kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, na Shekh Baasim Karbalai kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wakabainisha nafasi kubwa aliyo nayo msomi wa dini na majumu yake ya kuwaongoza watu katika njia ya haki hasa katika zama hizi zenye changamoto nyingi, bila kusahau jukumu la kufundisha dini katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: