Baada ya kumaliza kazi walizo pangiwa katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu wafanya kazi kadhaa zatika malalo ya bibi Ruqayya bint Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, na kwa msaada wa uongozi mkuu wa Ataba tukufu, ugeni wa Atabatu Abbasiyya –uliopo Sirya- umefanya matengenezo kadhaa katika malalo ya Sayyida Ruqayya bint wa Imamu Hussein (a.s).

Ugeni huo unahusisha watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram na mafundi miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka katika vitengo vingine, baada ya kumaliza utengenezaji wa sistim ya sauti na taa na vitu vingine katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), ndipo wakaelekea katika malalo ya bibi Ruqayya (a.s), ambako pia wamefanya matengenezo mbalimbali, miongoni mwa matengenezo hayo ni:

  • - Kusafisha kaburi tukufu.
  • - Kufunga sistim ya kamera za kisasa.
  • - Kufunga sistim ya taa katika kubba tukufu.
  • - Kufunga sistim ya taa katika milango ya haram tukufu.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa haram (bwana Hassan Hilali) ambaye ndio kiongozi wa ugeni huo ameumbia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya uongozi wa malalo ya bibi Ruqayya (a.s) kuongea na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, kutokana na ugumu wa mazingira waliyo nayo kwa sasa kiuchumi, Sayyid akatuagiza twende katika malalo ya bibi Ruqayya (a.s), na kufanya matengenezo tutakayo weza, hivyo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wamekarabati sistim ya taa za kubba tukufu, kwa kufunga zaidi ya taa (60) zenye mwanga mkubwa, pia wamefunga (Projecter) yenye uwezo wa mita (100) itakayo kua ikionyesha pembezoni mwa kubba, hali kadhalika wameweka taa katika milango ya haram na kuiwekea mkanda wa taa zenye rangi tofauti saba, pia wamelisafisha kaburi na kufunga kamera za ulinzi katika milango na ndani ya uwanja wa haram tukufu zipatazo (22) pamoja na mitambo iliyo onganishwa na kamera hizo”.

Kuhusu kazi wanazo tarajia kuzifanya siku za mbele (bwana Hilali) amesema kua: “Pamoja na kazi hizi, tumechukua vipimo vya milango ili tukatengeneze milango mizuri ya mbao inayo endana na hadhi ya sehemu hii na kuja kuondoa iliyopo na kuweka hiyo”.

Kumbuka kua safari hii imetumia siku (10), ndani ya siku hizo wamekamilisha kazi zote walizo takiwa kufanya katika malalo ya bibi zainabu na bibi Ruqayya (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: