Washiriki kupiga kura katika shindano la kwenda ziara kwenye Ataba tukufu za Iraq, na walio faulu wasema kua ilikua ndoto kwao na leo imekua kweli…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, lililo hitimishwa Alasiri ya Juma Mosi (19 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m), imeendesha zowezi la kupiga kura ya bahati nasibu kwa watu walio shiriki katika kongamano hilo kuanzia siku ya kwanza, ambao ni watu wa mji wa Karkal na maeneo yanayo uzunguka mji huo.

Ustadh Saamir Swafi mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Shindano hili ni moja ya vipengele muhimu katika kongamano, limepata mwitikio mkubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, na hili ndio lililo tuvutia kuendeleza shindano hili, awamu hii kuna marekebisho fulani yamefanywa katika shindano, na vimetengenezwa vitambulisho vya kura zaidi ya (2000) kwa kuzingatia kauli mbiu ya kongamano, kila kitambulisho kina nakala mbili, moja anapewa mshiriki na nyingine inabaki kwenye kamati”.

Akaongeza kusema kua: “Zawadi za washindi zina thamani kubwa sana kwa wapenzi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ambayo ni kwenda ziara katika Ataba tukufu za Iraq, nayo ni ndoto ya kila mtu usiku na mchana, hadi umekaribia wakati wa kuikamilisha kwa kushiriki shindano hili linalo kimbiliwa na makundi ya waumini wenye kiu kubwa ya kwenda kuzitembelea Ataba za Maimamu wao, na kunawirisha macho yao kwa kuangalia kubba zao tukufu, ukizingatia kua wengi wao bado hawajaenda ziara wanaziono kupitia luninga (tv) tu”.

Swafi akabainisha kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa zawadi ya washindi (20) na Atabatu Husseiniyya washindi (10) huku Atabatu Askariyya wakitoa zawadi kwa washindi (5), kila Ataba inagharamia safari za washindi iliyo ahidi kuanzia Karkal hadi Iraq na kuwatembeza katika Ataba tukufu”.

Wageni kutoka katika Ataba tukufu pamoja na wanachuoni wa mji huu na miji ya jirani walikua wanachukua kadi moja moja za washiriki baada ya kuchanganywa.

Walio bahatika kushinda walitokwa na machozi ya furaha na walishukuru sana kwa kupata fursa hiyo tukufu, isiyo lingana na utukufu wowote, ambayo ni kwenda kutembelea malalo tukufu za Maimamu nchini Iraq, wakasisitiza kua ilikua ndoto na sasa imekua kweli kwa baraka za Amirul Mu-uminina (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: