Rais wa ujumbe wa Atabatu Askariyya kwa watu wa Karkal: Tunashukuru kila moyo uliojaa mapenzi ya Hussein na kila chozi lililo toka kwa ajili yake…

Ustadh Naafii Jamali
Katika hafla ya kufunga kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita iliyo fanyika siku ya Juma Mosi (19 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m) katika hauza ya Ithna Ashariyya kwenye mji wa Karkal India, ambapo kulikua na ujumbe kutoka kwa wageni walio wakilisha Ataba za Iraq (Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) ulio wasilishwa na Ustadh Naafii Jamali ambaye ni naibu katibu mkuu wa Atabatu Askariyya, amesema kua:

“Hakika wakati mgumu zaidi ni wakati wa kutengana na watu unao wapenda, imepokewa kua (kitu kigumu kushinda kifo ni kutengana na unaye mpenda), leo tunakuageni kwa utukufu wa Manani asiye poteza tunayo tenda, baada ya kumaliza kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, ambalo tunatarajia kua tumefikia malengo yake, tunatoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikiwa kwake”.

Akaongeza kuasema kua: “Tunaushukuru kila moyo wenye mapenzi na Hussein na kila chozi lililo toka kwa ajili yake, tunamshukuru kila mtoto aliye kuja kwa ajili ya Hussein na kila mama aliye acha nyumba yake kwa ajili ya Hussein, na kila mzee aliye toka na kuja kwa ajili ya mapenzi ya Ahlulbait (a.s)”.

Akasema: “Nawakumbusha kua kuna amana ya Aali Muhammad (a.s) mliyo tekeleza, mmekuja bila kujali shida na matatizo ya safari, mmekuja bila kujali tofauti na mifarakano, mmekuja bila kuathiriwa na ushawishi wa Shetani, mmekuja kwa Aali Muhammad (a.s) kwa roho safi”.

Akaendelea kusema kua: “Tuna waaga na kujikumbusha wakati Imamu Mahdi (a.f) alipo muaga baba yake Hassan Askariy, na Hussein alipo muaga ndugu yake Abbasi, na alipo waaga watu wa familia yake, laiti mgekuwepo wakati Hussein (a.s) alipo ita akiwa peke yake: Je! Kuna msaidizi wa kutunusuru? Laiti mgekuwepo pale Shimri (maluuni) alipo kata shingo la Hussein, na wakati hema zilipo chomwa na kutekwa dada yake bibi Zainabu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: