Mheshimiwa Sayyid Kashmiri: Hakuna dawa ya ugonjwa wa balaa za kiroho na ubaguzi baina ya waislamu ispokua ni kufuata mwenendo wa Mtume na Imamu Ali (a.s)…

Sayyid Abu Hassan Almahdi
Katika hafla ya kuhitimisha kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, lililo fanyika Alasiri ya Juma Mosi (19 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m) katika hauza ya Ithna Ashariyya kwenye mji wa Karkal India, mwakilishi wa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Muhammad Baaqir Mussawi Annajafiy Alkashmiriy, alishindwa kuhudhuria kutokana na udhaifu wa afya yake hivyo ujumbe wake ukawasilishwa na mtoto wake Sayyid Abu Hassan Almahdi, ifuatayo ni nakala ya ujumbe wake:

“Salam kwa kila aliye hudhuria katika hafla hii tukufu miongoni mwa mafaqihi, wanachuoni na wakazi wote kwa ujumla, inanifurahisha kutoa pongezi za dhati kwetu kwa kufanya kongamano hili tukufu la kuhuisha kumbukumbu ya mtu aliye zaliwa ndani ya Kaaba tukufu kiongozi wa waumini Ali na Wasii ya Mtume mtukufu (s.a.w.w)”.

Akaongeza kusema kua: “Kongamano hili ambalo litaendelea kufanywa kila mwaka chini ya usimamizi wa kamati maalumu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hili ni jambo kubwa sana wanalo fanya kila mwaka hapa India, wakiweka mbele mambo ya kimataifa na kibinadamu ambayo ni sehemu ya mwenendo wa Imamu Ali (a.s), na kuangazia pande zote za dunia na kupambana na uovu na unafiki kila siku, hakika ujumbe wake ndio uleule wa Mtume (s.a.w.w) alio kuja nao kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, akamteua yeye auendeleze baada yake (s.a.w.w) kama wasii wake muaminifu na mlinzi wa kitabu na sunna, kama alivyo sema Imamu Ali (a.s), alitekeleza jukumu hilo katika uhai wake wote, pamoja na matatizo na madhila aliyo yapata sambamba na kuongezeka kwa maadui zake, lakini aliweza kutimiza wajibu alio achiwa wa kuongoza umma wa kiislamu”.

Akasisitiza kua: “Kuna umuhimu mkubwa sana waislamu wafuate mwenendo wake mtukufu, hususan katika zama hizi ambazo balaa la kubaguana kwa waislamu ndani na nje limekua kubwa, hakuna dawa ya ugonjwa huu ispokua ni kufuata mwenendo wa Mtume na Imamu Ali (a.s), Mwenyezi Mungu awabariki walio ita umma kwa ajili ya lengo hili tukufu, la kuunganisha waislamu na kusimama pamoja dhidi ya njama za kigeni zinazo endelea kua tishio kwa uislamu na waislamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawezeshe wasimamizi wa kongamano hili liendelee bila kusimama wala kupata pingamizi Inshallah”.

Akaendelea kusema kua: “Ilipangwa kufanyika kongamano hili kabla ya miaka miwili katika mji wa Kashmiri, lakini kwa bahati mbaya halikufanyika, pamoja na hivyo kamati inayo simamia imefanikiwa kulifanya katika mji wa Karkal, bila shaka utukufu unarudi kwetu wote hakuna tatizo, hakika waumini wa mji wa Karkal waliingia katika madhehebu ya Ahlulbaidi zaidi ya miaka mia moja iliyo pita, kutokana na utukufu wa mwanachuoni Muhammad, anaye julikana katika historia kwa jina la Amiru Shamsu Dini Al’iraqiy (q.s), ndiye mubaligh wa kwanza katika mji huu, katika kitongoji cha Karkal kuna kumbukumbu yake ya kudumu tangu wakati huo hadi leo, watu wa mji huu wanasifika kwa elimu, tabia njema na utekelezaji wa sheria, ukurasa wa historia yao umejaa majina ya wanachuoni wema, watu wenye zuhudi na ucha Mungu, inawezekana kutokana na sifa hizi tukufu Mwenyezi Mungu alitaka kongamano hili lifanyike katika mji huu, ni matarajio yetu mji huu utaendelea kua mfano mwema kwa miji mingine yote, natoa shukrani za dhati kwa wasimamizi wote wa kongamano hili kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: