Mahudhurio ya kiimani makubwa: Ufungaji wa kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita…

Sehemu ya hafla
Mahudhurio ya kiimani makubwa mmno, ndani ya mwezi mtukufu wa Rajabu Alasiri ya Juma Mosi (19 Rajabu 1439h) sawa na (7 Aprili 2018m) baada ya siku tatu zilizo jaa ratiba mbalimbali kuhusu kumuenzi Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kwenye kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Karkal India na kushiriki Atabatu Husseiniyya na Askariyya tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirul Mu-uminina ni wa mwanzo katika wenye kuabudu na mwenye zuhudi zaidi katika wenye zuhudi) kama sehemu ya kuhuisha na kukumbuka kuzaliwa kwa bwana wa Mawasii Imamu Ali (a.s), lililo fanyika katika hauza ya Ithna Ashariyya, na kuhudhuriwa na watu wengi sana miongoni mwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), walio anza kumiminika sehemu ya kongamano saa kadhaa kabla ya kuanza kwake.

Hafla ya kufunga kongamano ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomi wa Atabatu Husseiniyya bwana Falaah Zaliif, kisha ukafuata ujumbe wa Ataba tukufu zilizo shiriki katika kongamano, ulio wasilishwa na Ustadh Naafii Jamali naibu katibu mkuu wa Atabatu Askariyya tukufu, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika wakati mgumu zaidi ni wakati wa kutengana na watu unao wapenda, imepokewa kua (kitu kigumu kushinda kifo ni kutengana na unaye mpenda), leo tunakuageni kwa utukufu wa Manani asiye poteza tunayo tenda, baada ya kumaliza kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) la mwaka wa sita, ambalo tunatarajia kua tumefikia malengo yake, tunatoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikiwa kwake..”.

Ukafuata ujumbe wa mwakilishi wa Marjaa dini mkuu katika jimbo la Kashmiri Sayyid Muhammad Baaqir Mussawi Annajafiy Alkashmiriy, aliye shindwa kuhudhuria kutokana na udhaifu wa afya yake, mwanaye Sayyid Abu Hassan Almahdi akawasilisha kwa niaba yake, miongoni mwa aliyo sema ni: “Salam kwa kila aliye hudhuria katika hafla hii tukufu miongoni mwa mafaqihi, wanachuoni na wakazi wote kwa ujumla, inanifurahisha kutoa pongezi za dhati kwetu kwa kufanya kongamano hili tukufu la kuhuisha kumbukumbu ya mtu aliye zaliwa ndani ya Kaaba tukufu kiongozi wa waumini Ali na Wasii ya Mtume mtukufu (s.a.w.w)..”.

Wenyeji wa kongamano hili ambao ni hauza ya Ithna Ashariyya walitoa ujumbe wao pia ulio wasilishwa na rais wa hauza hiyo Shekh Naadhir Mahdi, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuchagua mji wa Karkal kua mwenyeji wa kongamano hili, pia akazishukuru Ataba zote zilizo shiriki katika kongamano hili na akasema kua hili ni tukio la kihistoria, litaandikwa kwa herufi kubwa katika historia ya mji huu.

Kisha likafanyika zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kushindania safari za kwenda kutembelea Ataba tukufu za Iraq, lililo ongozwa na Atabatu Husseiniyya na Askariyya..

Halafu zikatolewa zawadi kwa washiriki wa kongamano hili, viongozi wa Atabatu Husseiniyya na Askariyya pamoja na watu walio changia kufanikisha kwa kongamano hili.

Na mwisho kabisa alizungumza rais wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu, akasema kua: “Kuja kwetu katika ardhi hii kusinge kamilika ispokua kwa utukufu wa ushindi ulio patikana dhidi ya magaidi wa Daesh na kwa utukufu wa damu za mashahidi wa jeshi na Hashdi Sha’abi” kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: