Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, idara ya mahusiano na vyuo vikuu, ofisi ya harakati za shule siku ya Alkhamisi (18 Rajabu 1439h) sawa na (5 Aprili 2018m) wamefanya semina ya kujenga uwezo kwa walimu, yenye anuani isemayo (Mtambue mwalimu mwenye mafanikio) semina hiyo ilikua na washiriki (35) wakiwemo walimu na watumishi katika sekta za elimu.
Semina hii imefanyika katika ukumbi mkuu wa jengo la Imamu Hadi (a.s) lililo chini ya Ataba tukufu, ilichukua siku tatu mfululizo na kutumia jumla ya saa (16) kwa vikao vitatu, mkufunzi alikua ni Ustadh Azhar Abdulhussein Rikabi ambaye ni mkuu wa idara ya mahusiano na vyuo vikuu, mada yake ilihusu maendeleo ya kibinadamu na mbinu za kuamiliana na watu.
Semina ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukasomwa wimbo wa taifa sambamba na wimbo wa Ataba, washiriki wa semina hii wameshukuru sana juhudi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya elimu na malezi kwa kuwapa semina za mara kwa mara chini ya wakufunzi walio bobea katika sekta hii, pia ustadh wa maarifa ya Qur’an (Khaluud Muhammad) ambaye ni mshiriki wa semina alisema: “Hakika tumepata faida kubwa sana katika semina hii, masomo tuliyo fundishwa yanahitajika sana katika uwanja wa ufundishaji”.
Semina hii ni miongoni mwa juhudi za Atabatu Abbasiyya za kuboresha sekta ya malezi na elimu kwa ujumla na vituo vya malezi, kwa sababu ndio msingi wa kujenga mustaqbali na viongozi wa jamii katika kila sekta.