Kuendelea kupeleka misaada katika vikosi vya wapiganaji kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Kuendelea kupeleka misaada katika vikosi vilivyopo kwenye uwanja wa vita, uliondoka msafara wa misaada katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kamati ya maelekezo na misaada ya kitengo cha dini kuelekea katika miji ya Sanjaar, Huweija, Swalahu Dini hadi katika mipaka ya Sirya.

Msafara huo ulichukua siku nne mfululizo, walibeba kila kinacho hitajiwa na wapiganaji kwa kiasi walicho weza ikiwemo mavazi na chakula, ikiwa ni pamoja na kuwajenga kisaikolijia kwa kuwapa mawaidha na kujibu mwaswali.

Shekh Haidari Aaridhiy kutoka katika kitengo cha dini amebainisha kua: “Hakika misafara hii bado inaendelea, kabla ya siku chache tulitoka Karbala tukaenda hadi katika mpaka wa Iraq na Sirya kwa kupitia Mosul na mji wa Sanjaar hadi katika mpaka wa Sirya ulio pembezoni na mji wa Hasaka, tukabakia huko siku kadhaa, tukatembelea idadi kubwa ya vikosi vya wapiganaji waliopo huko miongoni mwa Hashdi watukufu, tuliwapa tulicho jaaliwa pamoja na kutoa maelekezo ya kifiqhi, tuliwafikishia salamu za Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, pamoja na wasia aliotoa kwa wapiganaji, vile vile tuliwafikishia salamu za kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akaongeza kusema kua: “Baada ya hapo tulitembelea kitongoji cha Sanjaar, ambacho kuna kikosi cha wabiganaji cha bibi Zainabu (a.s) chenye mafungamano na kikosi cha Abbasi cha wapiganaji, na tukaangalia mazingira wanayo ishi waumini, halafu tukaenda kutembelea mji wa Tal-Afar, ambao kuna wapiganaji wa kikosi cha Abbasi, kisha tukaenda katika wilaya ya Biji, tukatembelea wapiganaji wa kikosi cha Hassan Almujtaba waliopo huko, na tukasikiliza mahitaji yao na tukatoa msaada tulio jaliwa”.

Fahamu kua msafara huu ulifika hadi katika miji ya Riyadh na Huweija ambako kuna wapiganaji wa kikosi cha Ali Akbar, na kutoa msaada kwao, msafara ulimaliza ziara yake kwa kutembelea wapiganaji waliopo katika mji wa Swalahu dini eneo la Samara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: