Kufanyika mkutano wa kielimu wa kumi katika chuo kikuu cha Karbala kwa ushirikiano wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Juma Tatu (22 Rajabu 1439h) sawa na (9 Aprili 2018m) ndani ya ukumbi mkubwa wa kitivo cha utawala na uchumi katika mkoa wa Karbala, umefanyika mkutano wa kumi wa kielimu kwa ajili ya kutambua mahitaji ya msingi ya dira ya maendeleo hadi ufikapo mwaka 2030m na kujadili sekta ya uchumi.

Mkutano umehudhuriwa na viongozi wengi, akiwemo; waziri wa elimu ya juu na utafiti Dokta Muhsin Farifi, ujumbe ulio wakilisha Ataba mbili tukufu pamoja na jopo la watafiti wa kisekula wa kitaifa na kimataifa wanao jali jambo hili.

Mkutano ulifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wema wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa, ukafuata ujumbe wa rais wa kamati ya maandalizi Dokta Awadi Khalidi mkuu wa kitivo cha utawala na uchumi, akazungumzia ushindi walio pata wanajeshi dhidi ya magaidi wa Daesh, akaonyesha kua mkutano huu ni sehemu ya kuendeleza ushindi uliopatikana, kwani unawawezesha kuendelea kujadili mahitaji ya soko na kufanya mambo yanayo endana na malengo ya maendeleo endelevu.

Baada yake ukafuata ujumbe wa chuo kikuu cha Karbala, ulio wasilishwa na Dokta Muniru Saadi, ambaye alisema kua: “Leo kuna juhudi kubwa za kubadilisha utafiti wetu kutoka katika kiwango cha kitaifa na kuingia katika kiwango cha kimataifa, kwa kuangalia mahitaji mbalimbali ikiwemo lugha inayo faa kwa ajili ya mawasiliano ya kimataifa kutokana na utandawazi, hakika yanayo tokea Iraq yanakua na faida sawa kwa wote”.

Ukafuata ujumbe wa waziri wa elimu ya juu na utafiti Dokta Muhsin Fariji, akasema: “Tunaupongeza uongozi wa chuo kikuu cha Karbala na uongozi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kamati ya maandalizi, kwa kuandaa mkutano huu muhimu, tunatarajia matokeo ya utafiti wake yasaidie kutatua matatizo ya msingi yaliyopo katika sekta ya maendelea na uchumi wa Iraq”.

Kisha ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ulio wasilishwa na naibu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Bashiri Muhammad Rabii, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tuna haki ya kujifaharisha, sisi kama wairaq tuna urithi mkubwa kutoka kwa walio tangulia, tuna urithi mkubwa wa kiutamaduni, utamaduni wa Waadi Raafidina, utamaduni wa Somriyya Babelon Ashuriyya, na sisi kama waarabu na waislamu tunamiliki Qur’an tukufu na Ahlulbait (a.s) ambao ndio elimu ya kitabu”.

Akabainisha kua: Imamu Zainul-Aabidina (a.s) ana (kitabu) cha Risalatul Huquqi, kitabu hicho hakiwahusu waislamu peke yake, kinafundishwa katika vyuo vikuu mbalimbali duniani, kwa hiyo ni haki yetu kujifaharisha kutokana na urithi huu na msingi imara, tunao weza kuutumia na kutoka nao kwa walimwengi, hata katika zama zetu kuna wanachuoni wengi, kwa mfano Sayyid Muhammad Baaqir Swadr mtunzi wa kitabu cha Falsafa yetu na kitabu cha Uchumi wetu ambavyo pia vinafundishwa katika vyuo vikuu duniani”.

Akaongeza kusema kua: “Natamani kuona siku za mbele watafiti wetu na wanafunzi wa masomo ya juu tafiti zao zitokane na Qur’an au na watu wa mazingira, tuchukue kutoka huko yanayo tufaa katika ulimwengu wetu wa sasa”.

Mkutano ulipambwa na mambo mengi, ikiwemo kuangalia filamu inayo elezea harakati zinazo fanywa na kitivo cha utawala na uchumi katika chuo kikuu cha Karbala, na sababu zilizo pelekea kufanya mkutano huu, pia wahudhuriaji walipata fursa ya kuangalia maonyesho yaliyo andaliwa rasmi kwa ajili ya mkutano huu, mkutano ukahitimishwa kwa kujadili tafiti zilizo wasilishwa kwenye mkutano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: