Kuendelea kwa maandalizi ya kifundi na kihandisi katika eneo la maonyesho ya vitabu ya kimataifa Karbala…

Maoni katika picha
Kazi ya kuandaa eneo la maonyesho ya vitabu ya kimataifa yatakayo fanyika katika mji wa Karbala, inaendelea vizuri usiku na mchana, mafundi na wahandisi wanatengeneza sehemu yatakapo fanyikia maonyesho hayo, ambayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu lenye ukubwa wa (2m3000) yatakayo yatafanyika kwa muda wa siku (10), kuanzia siku ya (15/04/2018m) sawa na (28 Rajabu 1439h) hadi (25/04/2018m) sawa na (8 Shabani 1439h), maandalizi yamesha kamilika kwa zaidi ya asilimia (%60), sehemu ya maonyesho itakua na njia mbili kuu, ambazo zitakua na vibanda vingi vitakavyo tosha vituo vya usambazaji na taasisi zote pamoja na vyuo vikuu vitakavyo shiriki katika maonyesho haya, ambayo ni sehemu muhimu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada.

Mjumbe wa kamati ya maonyesho ya vitabu Dokta Hussein Mussawi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Maandalizi yalianza tangu mwanzoni mwa mwaka huu (2018m), mwanzoni mwa mwezi wa kwanza kamati ya maonyesho ya vitabu ilianza kufanya vikao na maandalizi ya maonyesho haya ambayo ni sehemu muhimu katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada”.

Akaongeza kusema kua: “Lengo la maonyesho haya ni kueneza moyo wa utamaduni katika jamii, na kurudisha vitabu katika nafasi yake ambayo ndio rafiki mwema, katika zama hizi za maendeleo ya kielektronik na vyombo vya mawasiliano ambavyo vinadhofisha nafasi ya vitabu, kwa hiyo maonyesho haya yanayo simamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya yanachangia kurudisha nafasi ya vitabu kama vilivyo kua zamani”.

Akafafanua kua: “Hakika vituo vya usambazaji vitakavyo shiriki katika maonyesho haya vinakaribia (150) vya kiarabu na kiajemi ukiongeza na vya hapa nchini, pia kuna vyuo vikuu vitakavyo shiriki, kikiwemo chuo cha Oxford (The University of Oxford), pamoja na taasisi za kiserikali zikiongozwa na wizara ya Utamaduni ya Iraq na vitengo vingi pamoja na taasisi mbalimbali zinazo jihusisha na sekta hii, vitabu vya aina zote vitaonyeshwa, kama vile vitabu vya dini, sayansi, utamaduni, vya sekula nk, vya kiarabu na visivyo kua vya kiarabu, kwani maonyesho haya sio ya mlengo mmoja, pia kutakua na ushiriki wa Hashdi Sha’abi katika maonyesho haya, watakua na tawi maalumu kwa ajili ya kuonyesha harakati zao, ambapo watawakilishwa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) na kikosi cha Ali Akbar (a.s) pamoja na vikosi vingine vya Hashdi Sha’abi.

Kumbuka kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa ambayo hufanyika katika mji wa Karbala, ni moja ya sehemu muhimu katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, linalo andaliwa na kugharamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, tangu lililo anzishwa miaka kumi na nne iliyo pita, kwa ajili ya kuhuisha mazazi ya mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), mwaka huu kuna ongezeko la nchi washiriki pamoja na vituo vya usambazaji, na wamewekewa vitu muhimu vitakavyo saidia kurahisisha maonyesho haya, ambayo huakisi mazingira ya kitamaduni ya Iraq kwa ujumla na hasa mji mtukufu wa Karbara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: