Kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha mlango wa haja, Atabatu Abbasiyya tukufu yawekwa mapambo meusi na yaandaa ratiba ya maombolezo…

Maoni katika picha
Katika kuhuisha kumbukumbu ya tukio linalo umiza la kuuawa kwa mfichaji wa hasira na mdhihirishaji wa elimu Imamu Mussa bun Jafari Kaadhim (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka mapambo meusi na imetangaza msiba, kuta na nguzo za ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zimefunikwa vitambaa vyeusi na kuwekwa mabango yaliyo andikwa riwaya mbalimbali zinazo zungumzia tukio hili, na bendera nyeusi zimepandishwa kwa ajili ya kuomboleza msiba huu na kumpa pole Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba ya kuomboleza ambayo inavipengele mbalimbali, pamoja na ushiriki wake katika kuwahudumia watu wanao kwenda kuwazuru Maimamu wawili Kadhimaini (a.s) katika mji mtukufu wa Kadhimiyya, kuhusu swala hili; kiongozi msaidizi wa idara ya usafirishaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Maitham Abdul-Amiri ameuambia mtandao wetu kua: Kitengo cha usafiri tangu jana Juma Tano (24 Rajabu 1439h) sawa na (11 Aprili 2018m) kimeanza kusafirisha Maukibu (vikundi) vya kutoa huduma kwa kutumia mabasi makubwa (12), safari zinaanzia katika eneo la Mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad) katika mji mtukufu wa Karbala kuelekea katika mji mtukufu wa Kadhimiyya.

Akaongeza kusema kua: pia kitengo hiki kimetuma mabasi (17) kwenda kushiriki katika kusafirisha mazuwaru kwenye kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Kaadhim (a.s), pamoja na mabasi ya kubeba maji na mengine ya kubeba gesi pamoja na kikosi cha mafundi walio jipanga kutengeneza gari lolote litakalo haribika katika kipindi cha ziara hii.

Akafafanua kua: Magari hayo yanafanya kazi mfululizo saa (24), kwa zamu mbili; ya asubuhi na jioni, ili kutoa huduma kwa mazuwaru wengi zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: