Kwa nyoyo zilizo jaa machungu… Maukibu ya waombolezaji ya pamoja ya Ataba mbili tukufu yampa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kifo cha Imamu Kaadhim (a.s).

Maoni katika picha
Kwa nyoyo zilizo jaa huzuni na machungu, Adhuhuri ya leo (25 Rajabu 1439h) sawa na (12 Aprili 2018m), yalifanyika matembezi ya kuomboleza ya pamoja kati ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, yaliyo husisha viongozi na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa saba miongoni mwa maimamu watakatifu, ambaye ni Imamu Mussa bun Jafari Kaadhim (a.s).

Matembezi yakiwa yametanguliwa na jeneza la kuigiza, yalianzia katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yakapitia katika uwanja wa katikati ya harama mbili tukufu, huku wakiimba kaswida na mashairi yaliyo amsha hisia za msiba huu uumizao, walipo wasili katika haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakapokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, kisha wakafanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), na wakaimba kaswida na mashairi yaliyo dhihirisha dhulma alizo fanyiwa Imamu Kaadhim (a.s).

Kwa upande mwingine: Maukibu za Husseiniyya zilianza kumiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu leo asubuhi, kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani wao ndio wenye msiba.

Fahamu kua Ataba za Karbala hufanya matembezi maalumu ya kuomboleza katika minasaba ya vifo vya Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: