Idara ya maji ya Atabatu Abbasiyya tukufu yatekeleza wajibu wake wa kunywesha maji mazuwaru wa Imamu Mussa Kaadhim (a.s).

Maoni katika picha
Kama kawaida yake katika kila msimu wa ziara ya kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s), idara ya maji chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya inatoa huduma ya kusambaza maji na kugawa barafu kwa Mawakibu (vikundi) vya kutoa huduma kwa mazuwaru chini ya ratiba maalumu na kushirikiana na kamati zingine zinazo husiana na maji.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Idara ya maji bwana Ahmadi Hanun, walikua na vituo vikuu vitatu katika sehemu zenye mazuwaru (watu) wengi na vilitoa huduma kipindi chote cha ziara, sehemu zenyewe ni:

Sehemu ya kwanza: Barabara ya Baabu Muraad.

Sehemu ya pini: Barabara ya Swahibu Zamaan (a.f).

Sehemu ya tatu: Barabara ya Imamu Ali (a.s). Katika sehemu hii tulifanya kazi kwa kushirikiana na Atabatu Askariyya tukufu.

Katika sehemu hizo tulisambaza vifaa vya kutunzia maji ya baridi pamoja na grasi za kunywea maji, sambamba na kugawa barafu na maji kwa mazuwaru na Mawakibu (vikundi) vya kutoa huduma kwa ajili ya kuwasaidia kugawa maji kwa mazuwaru watukufu.

Akaongeza kua: “Pamoja na kazi hiyo, pia tulisambaza maji kwa mawakibu zote zilizo kuwepo katika barabara zinazo zunguka haramu na katika uwanja wa Abdul-Muhsin Alkadhimiyya”.

Akabainisha kua: “Watumishi wa idara hii wamefanya kazi mfululizo tena kwa moya mkubwa, walikua wanashindana katika kutoa huduma, pamoja na msongamano mkubwa wa watu katika njia zote, hakika wamefanya kazi saa zote bila kubumzika na walikua na zamu mbili, ya asubuhi na jioni”.

Fahamu kua maji na barafu vimetoka katika kiwanda cha maji cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: