Idara ya kupotelewa ya Atabatu Abbasiyya inawaomba mazuwaru kuweka vitu vyao vya thamani kwenye vituo kwa ajili ya kujiepusha na kupoteza au kuibiwa…

Maoni katika picha
Vitengo na idara za Atabatu Abbasiyya tukufu zinafanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa malalo ya mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwemo idara ya kupotelewa ambayo ipo chini ya kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo inajukumu la kutunza mali za mazuwaru zilizo okotwa na kukabidhiwa kwao, na humrudishia mwenye nayo mara tu anapo patikana, mtandao wa kimataifa Alkafeel umekutana na kiongozi wa idara ya kupotelewa Sayyid Ahmadi Hamza, ambaye amesema kua: Hakika idara ya kupotelewa ni miongoni mwa idara muhimu ambazo zinafanya kazi moja kwa moja na mazuwaru, idara hii inajukumu la kutunza mali zilizo okotwa ndani ya haram tukufu au maeneo yanayo zunguka haram na kukabidhiwa kwao, ambapo hulazimika kumtafuta mmiliki wa mali hiyo na kumkabidhi mali yake kwa mujibu wa sheria, mara nyingi hutokea katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kwa hiyo tunawaomba mazuwaru watukufu wanaokuja kumzuru mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s), wakabidhi vitu vyao vya thamani kama vile hela, dhahabu na vingine kwa ajili ya kuogopa wasipoteze au kuibiwa.

Akaongeza kusema kua: Mali tunazo pokea hua tunazisajili na kuzipiga picha, kisha tunaziingiza katika orodha maalumu na tunazitangaza katika ukurasa wetu rasmi uliopo katika toghuti ya Atabatu Abbasiyya tukufu (mtandao wa kimataifa Alkafeel), kazi hii hufanywa kwa kutumia vifaa maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mali zote za thamani na kuzirudisha kwa wenye nazo, tangu kuanzishwa kwa idara hii hadi leo, tumesha rudisha mamilioni ya vitu kwa wamiliki wake, sasa imeongezwa idara nyingine ambayo inajukumu la kugawa vijitabu vya dua kwa mazuwaru watukufu, hivi karibuni umeanzishwa utaratibu wa kusajili vitu vilivyo okotwa kwa kufuata mpangilio wa herufi sambamba na kuandika maelezo yake katika kompyuta.

Tunapenda kuwakumbusha kua namba za idara ya kupotelewa iliyopo upande wa mashariki wa ukumbi wa haram tukufu, karibu na mlango wa Furat.

Namba: 322600 ya ndani: 141

Ufunguo wa nchi: 00964

Ufunguo wa mji: 032

Namba za mezani: 327999 – 333254 – 333253

Mawasiliano yetu: 009647400342201

Athiir: 009647804947331

Kiongozi wa idara: 00964801016727

Mawasiliano kwa barua pepe: lost@alkafeel.net

Kwa faida zaidi:

Ofisi ya kupotelewa ya Atabatu Husseiniyya tukufu (namba ya mezani): 324873

Ofisi ya kupotelewa ya eneo la baina ya haram mbili: 0096447602007666
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: