Utukufu na ibada za siku ya kupewa Utume (Mab’ath)…

Maoni katika picha
Siku ya Mab’ath ni siku aliyo pewa Utume mtukufu wa daraja Muhammad (s.a.w.w), ilikua Juma Tatu tarehe ishirini na saba ya mwezi wa Rajabu kabla ya kuhama Maka mwenda Madina kwa miaka kumi na tatu, na miaka arubaini baada ya mwaka wa tembo, sawa na mwaka wa (160 m), nayo ni siku tukufu sana, huzingatiwa kua ni miongoni mwa sikukuu muhimu katika uislamu.

Shekh Kaf’ami katika kitabu cha Misbaahu anasema: Imepokewa kutoka kwa Abu Jafari Jawaad (a.s) anasema: (Hakika katika mwezi wa Rajabu kuna usiku bora kushinda kila kitu kinacho angaziwa na jua, nao ni usiku wa tarehe ishirini na saba, katika siku hiyo Mtume alipewa (rasmi) Utume asubuhi yake, hakika mwenye kufanya ibada katika usiku huo miongoni mwa wafuasi wetu ataandikiwa thawabu sawa na mtu aliye fanya ibada miaka sitini), nao ni usiku wa maandalizi ya kupewa utume, ambayo ni siku tukufu sana, nayo ni miongoni mwa siku kuu kubwa, siku ambayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliijiwa na Jibrilu na kupewa Utume rasmi.

Katika usiku wa Mab’ath kuna ibada na dua zilizo suniwa:

  • 1-
  • 2- Kuswali rakaa kumi na mbili zilizo pokelewa na Imamu Muhammad bun Ali Jawaad (a.s).
  • 3- Kumzuru Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
  • 4- Kusoma dua isemayo “Allahumma inni as-aluka bitajalliy a’adham fii hadhihi llailah mina shahril-muadham…”

Siku ya tarehe ishirini na saba ya mwezi wa Rajabu Mtume (s.a.w.w) akapewa Utume rasmi, Mwenyezi Mungu mtukufu alimtuma Jibrilu (a.s) aende akamwambie kua yeye ni mtume wa watu wote na ndiye wa mwisho katika mitume..

Miongoni mwa ibada muhumu zinazo pendekezwa kufanywa katika siku hii ni:

  • 1-
  • 2- Kufunga, mwenye kufunga swaumu yake hua ni kafara ya miezi sitini.
  • 3- Kumswalia Mtume na Aali zake kwa wingi.
  • 4- Kumzuru Mtume wa mwisho na mbora wa Mitume Muhammad (s.a.w.w) na kumzuru Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
  • 5- Kuswali rakaa mbili, katika kila rakaa unasoma Alhamdu mara moja na Tauhidi mara (10).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: