Katika awamu ya nne: Mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa waanza kusajili watu wenye vipaji vya usomaji wa Qur’an na wanao penda kushiriki…

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa awamu ya nne, ambao ni moja ya miradi ya Qur’an inayo endeshwa na kituo cha miradi ya Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuanza usajili wa watu wenye vipaji vya usomaji wa Qur’an na wanao penda kushiriki.

Kamati imesema kua usajili ulianza tangu siku ya Ijumaa (26 Rajabu 1439h) sawa na (13 Aprili 2018m) na utaendelea hadi (5 Mei 2018m) chini ya kanuni zifuatazo:

 • 1- Maombi ya usajili yatapokelewa kupitia moja ya njia mbili: Telegram au Whatsap kwenye simu namba (07800119249).
 • 2- Kwa ajili ya kurahisisha usaji wa washiriki, kamati ya usimamizi ya mwaka huu imeamua kufanya usajili kwa aina hii:
 • - Msomaji atume rekodi ya usomaji wake aliosoma sehemu anayo penda na kwa mahadhi anayo penda, sawa yawe ya kiiraq au ya kimisri, rekodi hiyo iwe ya dakika moja na nusu hadi mbili, na awe amezingatia kanuni za usomaji.
 • - Rekodi hiyo iwe ya video, na aanze kwa kutaja majina yake matatu na jina la mkoa anako toka, asipo fanya hivyo ushiriki wake hauta kubalika.
 • - Atume ujumbe wa maandishi sambamba na kipamde cha video yatakayo kua na maelezo yafuatayo, asipo fanya hivi usajili wake hautakubaliwa:
 • 1- Majina yake matatu na laqabu (jina la sifa).
 • 2- Tarehe ya kuzaliwa kwake (siku – mwezi – mwaka) asizidi miaka (17), atakaye zidi umri huo hatakubaliwa.
 • 3- Jina la mkoa, wilaya au tarafa.
 • 4- Namba ya simu ya msimamizi wake, atakaye kua mdhamini wake katika usajili na atakaye thibitisha ubora wa tabia zake iwapo akikubaliwa.
 • 5- Jina la mwalimu wake aliye mfundisha kutoka katika mji anao ishi, awe mdhamini wake na athibitishe uzuri wa tabia zake iwapo akikubaliwa.
 • 6- Namba ya simu yake binafsi.
 • 7- Je! Amesha wahi kushinda katika mashindano yeyote ya Qur’an siku za nyuma? (andika jina la mashindano, mkoa yaliko fanyika, nafasi uliyo pata na tarehe).
 • 8- Picha ya mwombaji.
 • 9- Mazingatio muhimu:
 • A- Tunamshauri mshiriki aombe ushauri wa kuchagua njia sahihi ya usomaji wake, kwani iwapo atasajili kimakosa anaweza kushindwa kuendelea baada ya kutanihiwa na walimu wetu wa mradi huu baada ya kukubaliwa kwake.
 • B- Azingatie utamkaji sahihi wa herufi za Qur’an.
 • C- Maombi yatakayo tumwa zaidi ya mara moja kupitia namba tuliyo taja kwenye mitandao ya kijamii hayata kubaliwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: