Kituo cha Alkafeel cha matangazo mubashara kilicho chini ya kitengo cha elimu na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuandaa masafa maalumu ya matangazo bila kutumia alama ya (local) ya kurusha picha zenye ubora mkubwa kutoka ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mda wa saa 12 kila siku, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku, masafa hayo sambamba na picha yatarusha pia dua za kila siku, mihadhara ya kidini pamoja na shughuli zinazo fanyika katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vilevile kuna matangazo ya pamoja baina ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ya kurusha matukio ya pamoja kama vile adhana na khutuba za swala ya Ijumaa.
Kituo kikaongeza kusema kua, kikitaka kurusha shughuli ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kitatoa tangazo kabla ya shughuli kuanza, ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa vyombo vya habari vitakavyo penda kurusha, masafa hiyo inapatikana kupitia anuani zifuatazo:
SAT:INTELSAT 902@62°E
DL:11457.5V
SR:3000
DVBS2
PSK8
FEC 2/3
HD/MPEG-4
Kwa maelezo zaidi wasiliana na mkuu wa kituo cha matangazo kupitia namba ya simu ifuatayo (009647706007187).