Idara ya maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala yakutana na wawakilishi wa vituo na taasisi za usambazaji zitakazo shiriki na yawasisitizia kua: kwa kushirikiana kwetu tutapata mafanikio mazuri…

Maoni katika picha
Maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala ni moja ya sehemu muhimu za kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada, kamati ya maandalizi ya kongamano hilo huyapa umuhimu mkubwa maonyesho haya na imeyapa nafasi kubwa katika maandalizi yake.

Kutokana na kukaribia kuanza kwake, ambapo yataanza kesho Juma Pili (28 Rajabu 1439h) sawa na (15 Aprili 2018m), kamati ya maandalizi ya maonyesho ya vitabu ya kimataifa imekutana na wawakilishi wa vituo na taasisi washiriki.

Mkutano huo ulijadili mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo ya kanuni za maonyesho, na mengineyo miongoni mwa maelekezo muhimu katika maonyesho hayo.

Mkuu wa maonyesho haya Dokta Mushtaqu Muan Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika mkutano huu tumefafanua kanuni za maonyesho kwa ajili ya kujenga uhusiano mzuri na wadau wa maonyesho, kwa sababu lengo letu ni moja tu, nalo ni kuhakikisha maonyesho haya yanakua mazuri na kufikia makusudio, ambayo ni kurudisha mapenzi ya kusoma vitabu, hakika vituo vinavyo shiriki katika maonyesho haya vimeonyesha ushirikiano mkubwa na vimeahidi kutii na kutekeleza maagizo yote waliyo pewa na uongozi”.

Akaongeza kusema: “Aidha miongoni mwa mambo tuliyo ongea ni kuhakikisha tunakua na mazungumzo ya undugu baina ya idara na washiriki na baina ya washiriki wao kwa wao, na kuheshimu utukufu wa eneo hili, kusifanyike vitu vinavyo chochea ubaguzi na mfarakano au ambavyo haviendani na utukufu wa mji wa Karbala na Iraq kwa ujumla”.

Kumbuka kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa yataanza kesho, kuna jumla ya vikundi na taasisi za usambazaji (133) zinazo shiriki, kutoka ndani na nje ya Iraq, na ufunguzi wake rasmi utafanyika tarehe tatu Shabani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: