Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel lafanikiwa kutibu maradhi yaliyo shindikana katika hospitali za kigeni…

Maoni katika picha
Mafanikio mengine yapatikana katika hospitali ya rufaa Alkafeel, ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, jopo la madaktari wake limefanikiwa kufanya upasuaji wa kuondoa chembechembe za maradhi katika kichwa cha mtoto Zaharaa kutoka katika mkoa wa Dhiqaar, huu ni miongoni mwa upasuaji mgumu sana, kwani athari za chembechembe hizo ilikua imefika hadi kwenye ubongo.

Rais wa jopo la madaktari hao Dokta Ali Kanji amebainisha kua: “Jopo la madaktari limefanikiwa kuondoa chembechembe za maradhi katika kichwa cha mtoto mwenye umri wa miaka (12) katika upasuaji ulio chukua zaidi ya saa kumi mfululizo, chembechembe hizo zimejirudia rudia katika kichwa cha mtoto kutokana na maradhi ya kurithi yaliyo muanza tangu akiwa na umri wa miaka mitatu”.

Akaongeza kusema kua: “Mtoto huyu alikua amesha fanyiwa upasuaji mara saba katika hospitali za kigeni, nne katika hizo alifanyiwa Italia, kila alipo kua akitolewa chembechembe hizo zilikua zinaana tena, jambo lililo sababisha usumbufu mkubwa kwake, kwani chembechembe hizo zilikua zinasambaa kwa kiwango kikubwa ndani ya ubongo na upande wa jicho lake la kushoto, hadi jicho limetoka sehemu yake na kusababisha kuharibika kwa uso wake, upasuaji wote ulio fanyika awali haukufanikiwa kutokana na chembechembe hizo kua sehemu hatari sana na kuchanganyika na ubongo”.

Akaendelea kusema kua: “Katika upasuaji huu tulishirikiana na daktari bingwa wa macho kutoka Uturuki, Dokta Adnaan Aksuwi, ambaye alilirudisha jicho sehemu yake baada ya kuondolewa chembechembe za maradhi aliyo kua nayo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu hali ya mtoto kwa sasa inaendelea vizuri”.

Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kuanzishwa kwake imesha fanya mamia ya upasuaji wa aina mbalimbali, na asilimia kubwa walifanikiwa kwa sababu kuu mbili: kwanza, umahiri wa madaktari wake bingwa wa ndani na nje ya Iraq, pili, ubora wa vifaa tiba walivyo navyo, kwa kupatikana vitu hivyo viwili na baraka za mwenye jina la hospitali hii ambaye ni Alkafeel Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel unaweza kutembelea toghuti ya hospitali ifuatayo: www.kh.iq au piga simu zifuatazo: (07602344444) au (07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: