Kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (1000): Mradi wa Qur’an katika vyuo vikuu na Maahadi za Iraq wahitimisha program zake…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya siku ya Mab’ath (kupewa Utume) na kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (1000), Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya (Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya tukufu) zimehitimisha mradi wa Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, ulio endeshwa kwa kushirikiana na kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ya ufungaji wa program hiyo imefanyika katika jengo la Shekh Kuleini (r.a) ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi sambamba na idadi kubwa ya wanafunzi walio shiriki katika program hiyo na walimu wa vyuo.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na mwanafunzi wa mradi huu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na katibu mkuu Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar, akatoa pongezi kwa wahudhuriaji kutokana na mnasaba wa siku ya Mab’ath, akasema: “Kufuatia kumbukumbu hii tukufu Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’an imeamua kufanya hafla ya kuwapongeza wanafunzi walio shiriki katika mradi wa Qur’an tukufu, hakika Atabatu Abbasiyya ina miradi mingi, miongoni mwa miradi muhimu kwake ni kuwahudumia mazuwaru watukufu, hali kadhalika miradi ya kielimu, kibinadamu na kitamaduni, na inatilia umuhimu zaidi miradi ya Qur’an kwa sababu miradi hiyo unatumikia vizito viwili vitukufu kitabu na kizazi kitakatifu”.

Akaongeza kusemakua: “Hakika kitabu kitukufu ndio katiba ya Mwenyezi Mungu tunayo takiwa kushikamana nayo, harakati hizi za kushirikisha vijana tunazo ziona sasa hivi zinatupa moyo wa kufanya kazi zaidi, hatuna cha kusema zaidi ya kupongeza kazi hii tukufu na kuwatakia mafanikio mema, hatima ya mambo ya nchi hii ipo mikononi mwenu, na mfano mzuri wa hilo ni kazi nzuri iliyo fanywa na ndugu zenu wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi, Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wao na awalinde makamanda na awaponye haraka majeruhi wetu”.

Ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya Shekh Jawadi Nasrawi, ambaye alielezea miradi inayo fanywa na Maahadi ya Qur’an tukufu. Akabainisha kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya inaipa umuhimu mkubwa miradi inayo husu Qur’an tukufu, kila mradi unao pendekezwa unapasishwa na kupongezwa na kuomba ifanyike zaidi, Maahadi ya Qur’an imesha fanya miradi mingi kuhusu Qur’an tukufu, na kila mmoja ulikua na umuhimu wake katika kujenga uwelewa kwa jamii, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi huu, ulio lenga kundi muhimu katika jamii, ambalo ni kundi la wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, ambao walishiriki zaidi ya wanafunzi (1000) wa kiume na wakike, fahamu kua mradi huu umeendeshwa kwa ushirikiano baina ya Ataba mblili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.

Nasrawi akasisitiza kua: “Miaka ijayo kutakua na nadwa (darasa mjadala) kuhusu namna ya kutatua matatizo ya kielimu kwa kutumia Qur’an tukufu, ambalo ni tatizo kubwa linalo tishia imani ya mwislamu, hilo litasimamiwa na walimu bora na wenye utaalamu mkubwa, tunatoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikiwa kwa kongamano hili”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa wanafunzi walio shiriki katika mradi huu, ulio wasilishwa na bwana Sajjaad Hassan Awaadi, ambaye aliishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu hususan Maahadi ya Qur’an, kwa kuendesha mradi huu wa Qur’an unao jenga uwelewa zaidi wa kitabu kitukufu na kizazi kitakatifu, tunatarajia kuona miradi kama hii inaendelea kufanyika na kuwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq.

Ukafuata wakati wa kaswida za Husseiniyya zilizo husu kumbukumbu ya siku ya Mab’ath na mapenzi kwa mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), zilizo imbwa na kikundi cha kaqwida cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa sauti nzuru za kupendeza.

Baada ya hapo zikatolewa zawadi kwa walio changia kufanikiwa kwa mradi huu ambao umefanyika mwaka wa tano mfululizo, na kugawa vyeti kwa wanafunzi walio shiriki katika mradi ambao ulikua ni fursa muhimu kwao ya kujifundisha elimu bora zaidi yenye manufaa makubwa duniani na akhera.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: