Tupo katika siku za kumbukumbu ya kupewa Utume kwa Mtume mtukufu, tunapo kutana na kukumbuka jambo hili yatupasa kufahamu kua tunakumbuka siku ya kuzaliwa kwa uislamu, kwani uislamu umezaliwa katika siku hiyo, kama tumepokea uislamu katika siku ya kuzaliwa kwake, yatupasa kufahamu kua uislamu uliishi vipi katika siku zake za mwanzoni na namna gani Mtume (s.a.w.w) alivyo ukumbatia, na waislamu wa mwanzo walikua vipi, hakika kumbukumbu ya siku ya Mab’ath itaendelea kua mpya na yenye mazingatio makubwa, kupewa utume ni nuru na ndio kuzaliwa kwa uislamu na Qur’an tukufu, ilikua ni siku kubwa ya uongofu wa walimwengu.
Kutokana na hayo tuliyo eleza Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya imefanya hafla kubwa ndani ya uwanja mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hafla hiyo ilikua na sura ya kimashairi, wameshiriki washairi wengi akiwemo Muhammad Mussawi na Nasoro Karbalai, ambao waliburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kusoma mashairi yaliyo elezea utukufu wa siku hii, na kuelezea mazingira muhimu ya kihistoria ambayo uislamu uliyapitia na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) na mitihani aliyo pambana nayo katika kazi ya kufikisha ujumbe huu kwa walimwengu.