Kwa ushiriki wa zaidi ya vituo vya usambazaji (133): Maonyesho ya vitabu ya Karbala ambayo ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada yameanza…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Juma Pili ya leo (28 Rajabu 1439h) sawa na (15 Aprili 2018m) katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili lililo pauliwa, yameanza maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika katika mji wa Karbala awamu ya kumi na nne, ambayo ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ambayo yatafunguliwa rasmi mwezi tatu Shabani.

Maonyesho hayo yataendelea kwa muda wa siku (10) kuanzia siku ya (28 Rajabu 1438h sawa na 15/4/2018m) hadi tarehe (8 Shabani 1439h sawa na 25/4/2018m), katika maonyesho haya kuna zaidi ya vituo (133) vya usambazaji wa vitabu kutoka ndani na nje ya Iraq, kutoka katika nchi saba ambazo ni: (Uingereza, Lebanon, Iran, Misri, Jodan, Sirya na Iraq), ukubwa wa eneo yanapo fanyika maonyesho haya ni (2m3000).

Kiongozi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa dokta Mushtaqu Muan Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maonyesho haya ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa la Rabiu Shahada, hakika awamu hii itakua ya aina yake kutokana na aina ya vitabu vinavyo onyeshwa ambavyo vinalenga watu wa tabaka zote katika jamii, pamoja na mambo ya kitamaduni na elimu za kisekula na kidini”, akafafanua kua: “Kufunguliwa mapema maonyesho haya ni kwa ajili ya kutoa muda mrefu zaidi wa kujitangaza kwa vituo vya usambazaji”, akaongeza kusema kua: “Maonyesho haya yanahusu kila sekta, kamati inayo simamia maonyesho imechukua tahadhari kwa kuzuia aina yeyote ya vitabu vinavyo shambulia serikali ya Iraq au vinavyo chochea ubaguzi na mifarakano au kushambulia alama tukufu za dini au vinavyo fundisha mambo yasiyo kua na maadili, vipo vituo ambavyo vimeshiriki moja kwa moja na vipo ambavyo vimetumia mawakala, hali kadhalika Ataba zote zimeshiriki kutoka ndani na nje ya Iraq pamoja na mazaru za kishia na uongozi wa wakfu shia”.

Akafafanua kua, Maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala, hutoa fursa ya kuwasiliana baina ya watu wenye akili, elimu na tamaduni mbalimbali pamoja na kujenga uaminifu na mawasiliano kati ya taasisi hizo.

Kumbuka kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala ni sehemu muhimu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, linalo simamiwa na kugharamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu lililo anzishwa, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: