Kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Madina na kuelekea Maka…

Maoni katika picha
Katika siku kama hizi mwezi (27) Rajabu mwaka wa (60) hijiriyya, Imamu Hussein (a.s) aliondoka Madina na kuelekea Maka akiwa pamoja na watu wa nyumbani kwake na maswahaba zake, wakiwemo wake zake, watoto wake na dada yake bibi Zainabu kubra (a.s), wakapita njia ya jangwani yenye mchanga mwingi, Imamu Hussein (a.s) aliongoza msafara huo, akiwa ni mwenye kukabilina na vitisho vya watawala waovu, huku akikumbuka namna alivyo hama baba yake Imamu Ali (a.s) kutoka Maka kwenda Madina akiwa na wakina Fatuma, akiwa ni mwenye kukabilina na vitisho vya Makuraishi, msafara wake haukua sawa na misafara mingine ya kawaida, alisafiri usiku wa giza ili asionekane na akapita njia isiyo tumiwa na watu wengi, huku anasoma aya isemayo: (Basi akatoka, naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Akasema: Mola wangu Mlezi! Niokoe na watu madhalimu).

Imamu Hussein (a.s) katika moja ya ujumbe wake aliongea lengo la kutoka kwake, alisema: (Na hakika mimi sijatoka kwa shari wala kwa kuonyesha ushujaa, wala kufanya ufisadi au dhulma, hakika nimetoka kwa ajili ya kutafuta islahi katika umma wa babu yangu (s.a.w.w) nataka kuamrisha mema na kukataza mabaya, na kufuata mwenendo wa babu yangu na baba yangu Ali bun Abu Twalib).

Imamu Hussei (a.s) kabla ya kuondoka katika mji wa Madina alizuru kaburi la babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ziara ya kumuaga, alikua anajua (a.s) kua hatarudi tena katika mji wa babu yake (s.a.w.w) na hata zuru tena kaburi lake baada ya siku hiyo, na kwamba atakutana naye mbele ya rehma za Mwenyezi Mungu baada ya kutunukiwa shahada.

Imamu (a.s) alisimama karibu na kaburi tukufu akaswali rakaa mbili, kisha akaomuomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: (Ewe Mola! Hili ni kaburi la mtume wako Muhammad (s.a.w.w) na mimi ni mtoto wa binti yake, nimefikwa na mambo unayo yafahamu, Ewe Mola! Mimi napenda mema na ninachukia maovu, na mimi nakuomba ewe mwenye utukufu na ukarimu, kwa haki ya kaburi hili na aliye ndani yake, unichagulie lile unalo liridhia na linalo mridhisha Mtume wako).

Abu Mukhnaf anasema: (Hussein (a.s) alikwenda katika kaburi la babu yake (s.a.w.w) akalia, kisha akasema: Ewe babu yangu mimi naondoka jirani yako nikiwa sipendi (kwa kulazimika) kwa sababu nimekataa kumbaiyya (kumkubali) Yazidi ambaye ni mtu mlezu na muovu, akiwa anaendelea kulia akashikwa na usingizi, akamuona babu yake (s.a.w.w) akiwa amemkumbatia na anambusu katikati ya macho mawili, huku akumuambia: Ewe mwanangu ewe kipenzi changu, mimi nakuona baada ya muda mfupi utakua umetupwa chini umeloa damu umechinjwa ukiwa na kiu katika ardhi iitwayo Karbala, na maadui zako wanataraji shifaa (uwombezi) wangu, wallahi hawata pata uombezi wangu. Ewe mwanangu ewe kipenzi changu hakika baba yako, mama yako, bibi yako, kaka yako, ammi yako, ammi wa baba yako, wajomba zako, mama zako, shangazi zako wana hamu kubwa na wewe, hakika una nafasi kubwa sana peponi hauta ipata ispokua kwa kuuawa kishahidi, hakika wewe, baba yako, kaka yako, ammi yako na ammi wa baba yako ni mashahidi, mtafufuliwa mara moja na mtaingia peponi kwa shangwe na bashasha. Akaamka kutoka usingizini na akawahadithia watu wa nyumbani kwake, wakafunikwa na wingu zito kisha wakaanza safari).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: