Kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Kongamano la mwaka wa kwanza kuhusu khutuba za Imamu Hassan (a.s) laanza…

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na mwendelezo wa miradi yake ya kuhuisha athari za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), asubuhi ya Juma Pili (28 Rajabu 1439h) sawa na (15 Aprili 2018m), limeanza kongamano la kwanza kuhusu khutuba za Imamu Hassan (a.s), linalo endeshwa na kamati kuu ya mradi wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, kwa kusaidiana na ofisi ya malezi katika mkoa wa Baabil chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan (a.s) ni tunu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na wasii mfaswaha).

Katika kongamano hili kuna jumla ya washiriki (117) ambao ni wanafunzi wa kiume na wa kike kutoka katika shule za msingi na sekondari za mkoa wa Baabil, kwa ajili ya kuandaa hatua ya mwisho itakayo kua na washiriki wanafunzi wa kike (17) na wa kiume (11), katika hatua hii umefanyika mchujo maalumu kwa wanafunzi wa kiume.

Kongamano limehudhuriwa na ujumbe maalumu ulio wakilisha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na viongozi wa idara ya malezi ya mkoa pamoja na wanafunzi washiriki, lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq.

Ukafuata ujumbe wa kamati kuu ya mradi wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), ulio wasilishwa na Ustadh Muhammad Hussein Abudi, aliishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na kitengo cha habari na utamaduni kwa kusimamia shughuli hii inayo muhusu Imamu Hassan (a.s), na kuangazia maisha yake (a.s) kwa kuangalia khutuba zake tukufu, katika shughuli hii wameshiriki wanafunzi (117) wa kike na wa kiume kutoka katika mkoa wa Baabil, walio kuja kwa ajili ya kufanyiwa majaribio (mtihani) na kuwachuja hadi wabaki wanafunzi (28) wa kike na wa kiume watakao shiriki katika hatua ya mwisho.

Ujumbe wa kamati ya walimu uliwasilishwa na Ustadh Ali Fadhili Khafaji mkuu wa shule ya Waailiy, alianza kwa kuwakaribisha wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, akatoa shukrani za dhati kwa kufanyika kwa kongamano hili ambalo linaimarisha mapenzi ya Ahlulbait (a.s) akiwemo Imamu aliye dhulumiwa Abu Muhammad Hassan Almujtaba (a.s).

Baada ya hapo wanafunzi walio kua wamejiandaa kushiriki shindano hili wakaanza kuwasilisha walicho hifadhi miongoni mwa khutuba za Imamu Hassan (a.s), na mwisho yakatangazwa majina ya walio faulu na wakapewa zawadi kwa mujibu wa kanuni zilizo wekwa na kamati ya majaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: