Kwa uthibitisho: Kitengo cha maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya chawazuia wawakilishi wake wa mikoani kujihusisha na kampeni za uchaguzi…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetoa agizo kwa wawakilishi wake waliopo katika mikoa mbalimbali ya Iraq wasijihusishe na mgombea yeyote au mlengo wowote wa kisiasa, kikisisitiza kua kitengo hicho ni sekta inayo jitegemea kwa ajili ya kazi ya kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya peke yake.

Hayo yapo katika barua rasmi waliyo andikiwa viongozi na wawakilishi wa kitengo hicho, ifuatayo ni nakala ya barua hiyo:

Kwa kila kiongozi na mwakilishi wa kitengo.. Ni marufuku kujihusisha na mlengo wowote katika uchaguzi au mgombea yeyote au kusambaza picha na vipeperushi kwaniaba yake au ya mtu mwingine, sisi ni sekta huru, kazi yetu ni kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya, sio wapinzani wa yeyote, wala sio wafuasi wa yeyote, yeyote atakaye fanya hivyo atakua amevunja kanuni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: