Kamati ya misaada chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu inaendelea kusaidia wakimbizi, na imetoa msaada kwa wakimbizi waliopo katika hema za Amiriyya Faluja…

Maoni katika picha
Kamati ya misaada chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani bado inaendelea kutoa misaada kwa wakimbizi, chini ya utaratibu walio jiwekea, safari hii wamekwenda kusaidia wakimbizi waliopo katika hema za Amiriyya Faluja, kufuatia watu wa mji huo kuomba wasaidiwe kutokana na hali ngumu ya maisha waliyo nayo.

Rais wa kamati hiyo Sayyid Shahidi Mussawi ametuambia kuhusu msafara huo kua: “Baada ya kuwasili maombi ya misaada katika ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani, kamati yetu imesafiri kuja kuwasaidia, tumekua tukifanya kazi hii tangu wakimbizi walipo anza kupatikana, sawa iwe ni kwa maombi yao au bila maombi, tuna ratiba kamili tunayo fuata katika kugawa misaada, tutaendelea na kazi hii hadi mkimbizi wa mwisho atakapo rudi nyumbani kwake”.

Akaongeza kusema kua: “Misaada tuliyo toa imehusisha vikapu vya chakula (700) vikiwa na aina nane za vyakula, pamoja na nguo (2500) za watoto, kiongozi wa kamati ya misaada akishirikiana na kiongozi wa wakimbizi waliopo katika hema hizo walisimamia ugawaji huo”.

Akabainisha kua: “Wakimbizi wamemshukuru sana Mheshimiwa Sayyid Sistani kwa mwitikio wake wa haraka na kupeleka miaada kwa familia za wakimbizi zifizopo katika mazingira magumu, wakasema kua jambo hili linaonyesha namna alivyo na moyo wa uzazi, na anavyo wajali raia wa Iraq, wakasema: Hakika tuna imani kubwa na Marjaa dini mkuu ya kulinda umoja wa wairaq na namna anavyo wahimiza viongozi kuwajali raia wote, katika maelekezo mazuri anayo toa kupitia khutuba za Ijumaa, na kuwataka wawe mfano mwema katika kuhudumia wananchi, wakimbizi hao wakaomba wafikishiwe salamu na dua zao kwa Mheshimiwa Sayyid Marjaa dini mkuu”.

Kumbuka kua misafara ya kutoa misaada inayo fanywa na kamati ya misaada chini ya ratiba yao maalumu inaendelea, sawa iwe ni kwenda kusaidia wakimbizi waliopo katika hema au katika miji iliyo kombolewa, kwa ajili ya kupunguza mateso ya familia hizo na kuwafanya wahisi kua Marjaa dini mkuu ndio kimbilio sahihi la wairaq wote na kuondoa picha mbaya inayo tangazwa na maadui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: