Atabatu Abbasiyya yawapa zawadi washindi wa mashindano ya Qur’an kutoka katika Maahadi ya Qur’an kitengo cha wanawake na yawasisitiza kuongeza juhudi…

Sehemu ya hafla
Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa zawadi kwa wasomaji wa Qur’an wa Maahadi ya Qur’an kitengo cha wanawake kilicho chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu walio pata nafasi za juu katika mashindano ya Qur’an tukufu, kuhifadhi, kusoma na tafsiri, yaliyo fanywa katika Ataba tukufu na katika taasisi zingine za Qur’an, ikuwa ni sehemu ya kuonyesha kujali juhudi zao na juhudi za wasimamizi wao, na wamehimizwa kuongeza juhudi kwa ajili ya kuongeza ushiriki wao kitaifa na kimataifa.

Hayo yamesemwa katika hafla iliyo fanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kusoma Qur’an ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kulikua na ujumbe wa Ataba tukufu ulio wasilishwa na Sayyid Adnaan Mussawi kutoka katika kitengo cha dini, alianza kwa kuwapongeza walio fanya vizuri katika mashindano ya Qur’an tukufu pamoja na wasimamizi wao, kwa kufanya kazi nzuri ya kutengeneza kizazi chenye uwelewa mzuri wa Qur’an tukufu, akafafanua ulazima wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, pia aliwaomba washindi waendelee kuongeza juhudi katika kukihifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho yake.

Kisha ikafuata program ya Qur’an ya wanafunzi wa chekechea wa marafiki wa Alkafeel chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu kitengo cha wanawake cha Najafu, na mwisho wa program hiyo washindi wa mashindano ya Qur’an wakapewa zawadi zao ambao ni:

 • - Imani Nasrudini Qassim, mshindi wa pili katika shindano la tajwidi.
 • - Khaludu Baaqir Abdul-Amiri, mshindi wa kwanza katika shindano la kuhifadhi Qur’an nzima lililo simamiwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kilicho chini ya wakfu shia.
 • - Maryam Ahamadi Swadiq, mshindi wa kwanza katika shindano la kuhifadhi juzuu kumi za Qur’an tukufu.
 • - Khaludu Baaqir Abdul-Amiri, mshindi wa kwanza katika shindano la kuhifadhi Qur’an juzu ishirini.
 • - Radhiyya Abudi Abbasi, mshindi wa tatu katika shindano la kuhifadhi Qur’an juzu ishirini kwenye shindano lililo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu.
 • - Hauraa Muhammad Hussein, mshindi wa kwanza katika shindano la kuhifadhi Qur’an nzima.
 • - Zaharaa Hussein Abdu-Swahibu mshindi wa pili katika shindano la kuhifadhi Qur’an juzu kumi na tano.
 • - Maryam Ahmadi Swadiq, mshindi wa kwanza katika shindano la kuhifadhi juzu kumi.
 • - Zainabu Mujadu Swahibu, mshindi wa pili katika shindano la kuhifadhi juzu kumi.
 • - Dhuha Hussein Halo, mshindi wa tatu katika shindano la kuhifadhi juzu kumi.
 • - Fatin Sataar Kaadhim, mshindi wa pili katika shindano la tafsiri ya Qur’an.
 • - Hauraa Aamir Yasini, mshindi wa kwanza katika shindano la usomaji wa Qur’an.
 • - Afraa Hanuun Sultani, mshindi wa pili katika shindano la usomaji wa Qur’an, washindi hawa, walishiriki katika mashindano ya kitaifa ya wanawake yaliyo simamiwa na Atabatu Alawiyya tukufu.

Hali kadhalika katika hafla hii maustadhat na viongozi wa idara ya elimu wa Maahadi nao walipewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: