Mhakiki Shekh Mahmudu Daryaab Najafiy atembelea maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu na aizawadia juzu (30) za vitabu alivyo andika…

Sehemu ya ziara
Miongoni mwa mfululizo wa ziara zinazo fanywa na wageni mbalimbali wasomi wa dini na sekula katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi karibuni Mhakiki Shekh Mahmudu Daryaab Najafiy kutoka katika hauza ya Qum tukufu akiwa pamoja na Dokta Muhsin Ahmadi Hablumatin walitembelea maktaba hiyo.

Shekh Najafiy alitembelea sehemu za maktaba na akasikiliza maelezo kuhusu vitu vilivyomo katika maktaba hiyo na bidhaa zinazo zalishwa nayo ikiwa ni pamoja na majarida mbalimbali, akakagua mitambo inayo tumika katika kuhakiki na kulinda nakala kale sambamba na upigwaji wake wa picha na namna ya kuzififadhi, ambayo ni mambo makubwa na muhimu katika sekta hii.

Baada ya kuridhishwa na alicho kiona Shekh Najafiy aliizawadia maktaba juzu (30) za vitabu alivyo andika ambavyo ni:

  • 1- Sanadi za kitabu cha Kaafi.
  • 2- Sanadi za kitabu cha Fiqhi.
  • 3- Sanadi za kitabu cha Tahdhibu
  • 4- Maelezo ya aya tukufu ya Burjadiy.

Mwisho wa ziara yake Shekh Najafiy alionyesha kufurahishwa na alicho kiona katika maktaba hii, akaomba huduma hii iendelee kwa faida ya dini ya kiislamu na madhehabu ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: